MNANIONEA BUREEEE……

Mweeeh, sasa naona natumiwa na waoga waliotaka kusema nilichosema ila wanaogopa so wanafikisha message zao kwa muhusika kwa kunitoa mimi kafara….hahahaha

Jamani, mmenitukana sana leo matusi mazito mengine nimeshindwa kurusha comment.

MMENIITA MNAFKI, sijui nini kila kitu eti kisa nimesema nimeamua kuacha kuongea mabaya juu ya CCM, wabunge wake na wagombea urais wake.

Wengi wamedhani eti nimejitoa katika vita sababu eti nimenunuliwa  au nimetishiwa …. sijatishiwa na mtu yoyote  na wala sina mtu nnae mwogopa dunia hii zaidi ya Mungu . Siwezi kumuogopa binadamu eti sababu ana pesa au sababu ana power nchini kwangu,yeye sio Mungu, binadamu hawezi kunifanya lolote lile. Ntakufa siku Mungu aliyonipangia sio siku binadamu atakayotaka….

Naomba kurudia tena, nimeamua kuachana na hii vita dhidi wya viongozi feki wa Tanzania sababu kuna issue imeibuka jana ambayo imeibua isssue ya conflict of interest. So I have to stay away……

Nimeumizwa sana na matusi yenu fans wangu pamoja na wasomaji wangu, yani kweli mpaka leo hamjanijua mimi ni mtu wa namna gani? Kweli mimi ni mtu wa kununuliwa au kuogopeshwa????? Sina utajiri mkubwa ila ALhamdulliah maisha yangu yanaridhisha, nimesoma nna elimu nzuri najua kuhangaika na nina mume anaejua majukumu ya kulea familia. Sina shida ndogo ndogo kiasi kwamba ntaacha utu sababu ya pesa. Sina tamaa ya pesa na sitakaa kuja kuwa na tamaa ya pesa sababu nimelelewa kwenye pesa, nimekulia kwenye pesa, naijua pesa so hainistui kabisa yani….

So nawaomba tena kwa mara ya mwisho, naomba muwe patient naomba mue wa subra wapenzi wangu…mTakuja kuelewa kwanini nimechana na hii vita….

Mimi na nyie tuko same side…..Sijahama team. Im still team ukweli na uwazi…… ILA limekuja swala la conflict of interest …..Its just not ethical for me as a blogger to continue this war….

Pia nimeshangaa sana watu wa Chadema wananichamba eti traitor, Chadema mnikomeeeeee kabisa mimi sio Chadema supporter mimi ni mwana CCM toka nimezaliwa mpaka leo na sijawahi kusema sikipendi chama changu sasa nashangaa mnataka kunitumia mimi kupigana na ccm , mimi siko against CCM mimi niko against  vitendo vya viongozi wengiii wa ccm hususan hawa waliopitisha SHUT UP TANZANIA LAW. PAMOJA NA MAFISADI…

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDU (BILA MABEPARI WA SHUT-UP TANZANIA LAW NA MAFISADI)……

“Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai.  Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma  tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa  kwa ugoni Kaisari  akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope  halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.”  – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere,

Kama BABA WA TAIFA , Nyerere alimkataa mwaka 1995 kwanini sisi vijukuu wa Nyerere tumkubali 2015???…..Ni nini kilichobadilika toka 1995 mpaka 2015 zaidi ya matukio ya kuprove Nyerere was right in 1995?  #Richmond

KWAHERINI

PS: NAOMBA TUENDELEE NA STORY ZA KINA DIAMOND NA MIMBA YA ZARI HUMU NDANI NA TUACHANE NA MAMBO YA SIASA…PLEASE MTANIELEWA BAADAE, TRUST ME. SIJAFANYA KILE MNACHODHANI NIMEFANYA…. ILA IMEBIDI NITUMIE BUSARA , NA NYIE BAADAE MTANI SUPPORT KWA HILI……NAOMBA TUWE PATIENT….

Read More

LE TAMKOZZZZ ……………

Wapenzi kuna habari nimezipata leo hii ambazo kwa kweli zimenifanya niache kuwa attack CCM na wagombea wao wa urais.  Hapana sijatishwa Wala kununuliwa na mtu yoyote yule. Ila imebidi nichukue uamuzi huu kutokana issue ya conflict of interest na kwamba naona Nikiendelea na hii vita huko mbeleni ntaonekana ni mnafki.

Kama mjuanvyo mimi ni mwana CCM wa damu. Ccm Iko damuni mwangu so naomba ieleweke Kuwa yote niliyoyasema humu niliyasema kwa uchungu mkubwa na mapenzi kwa nchi yangu na chama changu na sababu hizo hizo za mapenzi na nchi yangu ndo zilizonifanya niache kuwajadili wagombea urais wa CCM…

Although taarifa hiZi zimenifanya niachane na mpambano huu dhidi ya ccm na wagombea urais wake ila pia taarifa Hizi zimenifariji na kunipa hope kubwa mno na Chama changu. Soon mtanielewa. Yani kuanzia leo nalala usingizi mnono najua one day kila kitu kitakwenda sawa. Please msichukie wala kuniona traitor very soon mtanielewa na kunipongeza kwa msimamo huu. 

Kama mnavyonijua mimi sipendi unafki wala uonevu na soon mtajua Kuwa hizi principles mbili ndo zilizonifanya nichukue uamuzi huu mgumu.   Kidumu Chama cha mapinduzi

PS: Nawaomba muwe na subira wapenzi, pls vuteni subra soon mtaelewa na naamini mtaona busara yangu kwa kuchukua uamuzi huu…Yes nimeedit maneno makali niliyoyatumia kwenye posti za nyumba

Read More

VITA DHIDI YA SHUT-UP LAW – MENGI NA ROSTAM AZIZ WAKUMBATIANA……

 

Kimenukaaaaaaa, mpaka Mengi na Rostam wamekumbatiana katika kuongeza nguvu ya kuipinga shutup law…..

Unaambiwa hivi the enermy of my enermy is my friend….lol……

Ndo maana mie nilikuwa nawashangaa mburulaz wanaosupport shut-up law eti kisa Mange haisupport na wakati na yeye mwenyewe 

ni victim wa shut-up law….Ona watu wanaojua kutafuta pesa na kulinda maslahi ya biashara zao wameona bora wapatane ili waongeze nguvu za kupigana na adui…..

Read More

MZEE MENGI ALALAMIKIA SHUTUP LAW KWA UPANDE WA VYOMBO VYA HABARI….

Tuachane na habari za walalahoi wa instagram naomba tuingie kwenye habari za kujenga taifa …plsss

Kina Mange tunaambiwa tunalalamika sana maana tunapenda kutukana watu mitandaoni

sasa Mzee Mengi anatukaaga watu mitandanoni eeh???

Jamani ni hivi nyie hamuelewi how serious this thing is….

Ni kwamba sio kwamba wametubana watu wa kwenye mitandao tu jamani hata maTV wanakaribia kupitisha na  sheria za kuwabana

eti hakuna tena independent news, eti wakat iwa taarifa za habari eti wanatakiwa waji connect na tv ya taifa ya TBC so habari zao ziwe

zimefanana na haabri za serikali…

Yani wabunge wa CCM wanatuchezea akili zetu jamani……

Jamani nimewachukia  wabunge  wa CCM mpaka basi  maana nimeambiwa hawa ndo bado viherehere huko bungeni eti wanataka huu mswada upite…. KHA!!!.Hivi ni kwanini watu wanakuwa na tamaa hivi jamani?

why wanakuwa cruel kiasi hiki? Yani kweli jamani wamebana mablog ,matav magazeti kila kituuuu.HIVI TUNAELEKEA WAPI?

YANI KUNA TOFAUTI GANI SASA NA KUISHI GERMANRY UNDER NAZI RULE????

Mzee wa forbes millionares alirusha tweet hiyo 2 weeks ago katika kutoa support ya cyber crime……

Jamani wewe kama ni Mtanzania, take action.  Kama by October shut up law na  na hii mpya itakuwa imepitishwa jamani lets vote for the opposition

tena tuombe assistance ya international parties kuja kumonitior elections ila kura siziibiwe….

Yani we have to drop them……..

HAPANA AISEE , THIS IS TOO MUCH NOW  Yani mie nilidhani ni mablog tuu ndo tumeekewa shutuplaw kumbe mpaka matv wanataka kuwekewa same law , mtanzania jiulize CCM wamepanga kitu gani jamani…..

WE JIULIZEEE KUNA NINI JAMANI UCHAGUZI HUU….HALI IMEKUWA MBAYA SANA….

Read More

ZAMARADI MKETEMA – OMG, SIJAWAHI ONA CELEB WA KIBONGO KAPENDEZA HIVIIIII……………

Huyu mwanamke katoka kuzaa juzi sidhani kama kamaliza hata mwezi toka ajifungue…uwiiiii,watu na miili yao

OMG, Now this is a hollywood  red carpet quality gown………

Unajua sasa hivi wabongo washakremisha kuwa lazma uvae nguo designed by ndo uende kwa red carpet

Nguo iwe mbaya au nzuri ili mradi designed by,kitu mbacho sio kweli maana kwa bongo hizo nguo zinashonwa na fundi Juma

na fundi Juma hata siku moja hawezi kushona nguo kama hii……

Im not trying kuwaharibia watu biashara au kula hapana ila ni kwamba kuliko umlipe designer hizo laki 8 sijui milioni akushonee nguo kwa fundi Juma kwa nini usimpe pesa hizo hizo ila umwambie akuagizie bonge la evening dress.

Jmani nguo ya ready made ni ya ready made tu huwezi linganisha na za fundi Juma…..

Wenzenu mastaar wa mbeleez wanavaa nguo za designed by because nguo ni nzuriiiiii balaaaaaaaaaaaaa yani sio za kwa fundi Juma…

Ndo maana mastar wa bongo siku zote kwenye red carpet kupendeza huwa tabu sana maana siku hizi wote wamesha kremisha kuwa lazma nikashone nguo kwa flani bila kujua kuwa ni nguo ya fundi ambae hata mtaani kwenu yupo anaweza kuishona tu ukimuelekeza vizuri na ukanunua kitambaa kkoo au downtown…..hahahahahahhaha….

So mpe designer wako hiyo million yako mwambie akutafutie nguo kama hii ya zamaradi hii nguo yani huulizi unajua kabisa fundi Juma hajashona…

So unampa pesa yako akuagizie nguo sababu umeshajua ana taste nzuri ya nguo so atakuletea nguo ya maana…..

Maana ona Zamaradi hakuvaa nguo ya kushonewa na mtu na akawafunika wooooooote……

Sasa bora hawa mastaa watu wa send off je? Yani mtu anavaa mgauni local alafy mshoni ni huo huo kama uniform kasoro vitambaa tu

alafu kwa pesa hiyo hiyo angeweza kuongea na huyo designer wale akaletewa nguo ya maaana hata kama designer atasema kaidesign yeye mtajuana wenyewe ila atleast muanze kuvaa nguo quality jamani harusi ni kitu cha maana sana…

Sherehe ambayo naona lazma ushone kwa designer ni Kitchen party tuuuuu sababu ni kitenge ila hizo zingine dah ni kituko… Alafu kama uniform no creativivty mshono huo huo…. Oneni sasa ambao hawafati mkumbo….

Muke ya Boss ulipendeza aiseeee……….

Read More
1 2 3 147
Designed by muzemultimedia web design Tanzania