X’MAS 2014…..

Hubby and his mommy….

Hubby’s family is here for the holidays……Last yr tulikuwa kwao this yr tumewaambia waje kwetu….

Last night we went to Malibu to dine at the amazing Gladstones seafood restaurant….

#FAMILYOVEREVERYTHING

Happy people….

Kama huna shangazi wa kukunywesha maji basi pole….lol..

Kenzo na shangazi Tate….awwww…

Moi…. Yani my hubby’s  family wameniambia hawajawahi kuniona nimependeza kama hivi nikiwa na short hair…lol..

Keany and mommy…..

my love…

Kenzo, mommy and daddy….

random pic…..lol..

Babu, Tate and Kenzo…

Babu and Keanu…

Busu la babu…. awww

KENZOKI…

Keanu is like “mommy pick me up” lol…

jamani mwanangu eti ndo kwanza kijino cha kwanza kinatoka…hahahhaha

Ila kameanza kusimama dede alafu kanaanguka…lol…

Dinner with hubby’s amazing family @ gladstones in Malibu….

Embu muoneni Keanu alivyo pose kwa picha…hahahahha

Keanu and Aunty.. Mapenzi tele….

Awwwwwww….

Muke ya muzungu…

IM HAPPYYYYYYYYYYYYYYYYYYYYYY……

Uwiii nimepiga diet nzuri last week mpaka vimikono vimepungua…lol…

Bibi, Kenzo and I…

My mother -in-law is an amazing woman…

Omg, I just love my father -in-law. The kindest man ever….

THESE ARE MY PEOPLE….

LEO X’MAS DAY TUMEKAA HOME ,TUME WATCH MOVIES ALL DAY……

WE ARE SURROUNDED BY SO MUCH LOVE……. THIS IS WHAT THE HOLIDAYS SHOULD BE LIKE…

Read More

JINSI YA KUFUNGUA PROFILE ON WWW.MATCH.COM

 Uwiii the response to online dating has been overwhelming and confusing…. Yani wengi wametuma pesa kwenye Mpesa yangu then ndo wananitumia text kuwa niwape username and password. Wapenzi simfungulii mtu profile… Uwiii maana sasa hiyo ni kazi haswaaaa…. Wengine wananitumia message kuwa wanashindwa kufungua profile coz waambiwa waingize zipcode na huku hawana zipcode……

Wapenzi simfungulii mtu profile coz its time consuming and Im very busy…… Kama utataka nikufungulie profile nikuandike maelezo yote etc chief ntaku charge one time cost ya $100. Kuliko kuchajiwa hiyo $100 si bora ufanye mwenyewe tu coz its very easy..

sasa nawapeni step by step info on how unaweza kufungua profile…. Kama bado unaona huwezi niambie nikufanyie ila ndo ntaku charge maana itabidi niache kufanya biashara yangu nikae nafungulia watu dating profile…. TIME IS MONEY MY FRIENDS…..

I will try to make this as easy as possible so you can do it yourself.

kwanza ukiingia tu kwenye website hii page ndo inakuja juu…..

Either click pale juu kushoto palipoandikwa member sign in au hapo panapotaka zipcode ingiza 90069 au ingiza any zipcode ya marekani..

uki google USA zipcode utapata zipcode elfu kidogo, ingiza tu alafu click view photos. Au click tu member signin zote zitakupeleka kwenye same page

Ukiletwa kwenye page hii  clock hapo chini kabisa palipoandikwa join for free.

utaletwa hapa. Hapa tena zipcode ingia any zipcode ya usa au ingiza hiyo 90069

utaletwa hapa uingize email address. Ingiza email yako. ingiza email yako ya ukweli maana wala haitoonyeshwa kwenye profile yako

na pia communications zote utatumiwa huko na pia itabidi uingie kwenye email yako ili u activate account yako. So weka email ambayo una access nayo

Hapa utaambiwa uingize username unayotaka kutumia. USIWEKE your real name.

Weka jina lolote lile unalotaka kutumia. kama hilo jina tayari lina mtu analitumia watakukatalia mpaka uingize jina ambalo hakuna mtu anatumia

then utapelekwa kwenye mapage mengine kibao ya kuweka personal information zako kibaaaa…. Kuwa mkweli kwenye hizo informationa.

Kama una mtoto andika. Ukimaliza huko utaletwa kwenye hii page. hapa mtu anaweza kuboogy akasema ukacheck kuwa unataka mwanaume mwenywe mshahara huyo wa $150k and above. Dont do that mistake. ofcourse unataka huyo mwenywe huo mshahara mkubwa ila usijionyeshe ugold digger wako mapema hivyo. Wanawaume wengine wenye pesa wako makini hawataki wanawake watakaowapenda sababu wana pesa so akiona mwanamke anaetaka mwanaume mwenywe pesa atakukimbia. Hapo kwenye salary chagua option ya no preference.

Headline yako pia ni important. Kuna headline nyingi kama “Looking for love”

usijali andika chochote utaweza kubadilisha baadae.

Then kwenye picha. Lazma uweke picha , profile sisizo na picha huwa hazipati response. utadoda humo.

Ila sasa kwa vile sisi wabongo ni wambea mnooo weka picha ambazo huzitumii kwenyw social media. yani usiweke picha zizle zile kama kwenye instagram au facebook yako.Weka ambazo hazimo kwenye insta yako. hata mmbea somehow akikutana na profile yako hatokujua fasta fasta…lol..

This is important… sasa kumbuka mpaka sasa hivi profile yako itakuwa inaonyesha kuwa wewe unaishi marekani, so inabidi ubadilishe location.

Hutaki profile yako ionyeshe uko marekani ,mwanaume aku contact alafu umwambie hapa nipo Africa. Utamboa…. So unabadilishaje location yako?

Cheki hapo juu kushoto nimehighlight , click kwenye settings

ukisha click kwenye setting utaletwa hapa. Ukifika hapa click location.

Uki click location utaletwa hapa. Click hiyo drop down menu chagua Tanzania, ukisha click Tanzania utaletewa miji yooooote ya Tanzania. Then choose mji…

Ila sasa ngoja nikupe ushauri.  Wabongo sisi ni wambea mno na tunapenda kufatiliana. N hii match.com haina siri wanaruhusu watu hata ambao hawajalipia membership,yani mwenywe free profile tu kubrowse profile za watu wengine.  Ila tu ni kwamba kama hujalipa huwezi kuwaisliana na mtu. Unaweza kucheki profile tu but no contact at all.  Sasa kwa vile watz sisi ni watu wa kufatilia na mtu asije kukuanika  usiweke Tanzania kama nchi yake , weka any other country kama Kenya au Uganda au South Africa. Ili mradi uwe Africa. Hata mmbea akitaka kujua watanzania gani wako kwenye hii website asikupate profile yako ng’oooo na hata akienda hizo nchi zingine kukutafuta uwiii mpaka apate profile yako ni bahati na sibu ya taifa. ila kwa vile watz wachache wako kwenye hii website ni rahisi sana mtu kukumbana na profile yako. So kama ni mke wa mtu au gf wa mtu na utaka kujiunga humu ili uachane na marioo wako ushajua trick choose another african country as your location then ukianza kuchat na jamaa mpya unamwambia uko Tanzania  ila tu match.com hawakukupa option ya kuchagua Tanzania…hahahahhaha…..maana ukianza kuji explain sana atakushangaaa bora uwasingizie match.com hawana option ya TANZANIA as a country….

sasa ukisha fanya hilo then hapo ndo binti Kimambi napohusika… Maana mpaka sasa unakuwa na profile ila huwezi kumcontact mtu na mtu hawezi kuku contact na hata mtu akikutumia message huwezi kusoma so its useless. Hapo ndo unitafute whatsapp +1 305 498 3696 unipe username yako na password then mie ntaingia ntakufanyia payment kwa credit card yangu then utaendelea ku hunt….. Sasa sio udanganywe upate mtu wa kwanza tu then akwambia anakupenda then ujitoe match fastaaa nope. Endelea kuhunt maana labda kuna better than him,usijitoe fasta bora hata ufungue profile mpya uendelee kuhunt ili usijitoa sbabau ya mwanaume wa kwanza tu…maana sisi wadada tukiambiwa I love you basi kila kitu tunasahau…hahahahha

Jamani hii kitu sio kwa wadada  tu  wanaotafuta wazungu tu, hii website ina watu wa rangi zote. Hata mnaopenda black wamejaa kibao humu. Pia matumizi ya hii website sio kwa wadada tu hata kwa mariooo wanaweza kutumia kupata mijimama ya kizungu itayotafuta wanaume wa kiafrica wenye mitalimbo ya haja….hahahahahha…. Tena jifanye mmasai ,vaa guo la kimasai piga picha weka humo yani siku mbili tu lazma jimama la kizungu likutumie message. Upelekwe ulaya  ,jifnaye fala umuone akupe makaratasi then ingia zako kitaa, au labda uta fall in love kabisa na jimama lako. Who knows!!

Yani ma kaka mahandsome boy jiwekeni humu na nyie mijimama ya kizungu itawapandisha pipa tu…. Kuna watu huku wako very lonely….lol..

Also ukiwezea kulipia membership ya hata 3 months ndo mwake zaidi, nakulipia kabisa 3 months then utanisahau na mie nakusahau sio kila mwezi unanitafuta nikulipie… Ila kama huna pesa ya 3 montsh uskonde ntakulipa ya 1 month.

Website hii wanacharge $40 kwa mwezi mimi ntakucharge dola $60 kwa mwezi,.kwa rate ya leo ni TSH 105,000

PS: Ushauri wa bure. Take your time kujibu maswali yooote na jaza profile yako vizuri. Usiwe na haraka. Na sehemu z akujieleza kwa maneno yako mwenywe au sehemu za kuelezea unataka mwnaume wa aina gani tafadhali usiandike kwa broken english, bora hata umuombe mtu akurekebishie hiko kiingereza ndo uweze. Dont turn him off kwa broken english juu ya profile yako… Its okay mkianza kuwasiliana ukawa na broken english ana jua wewe ni mwafrica english ni second language ila profile yako kuandikwa in broken english ni very tacky. 

Read More

JINSI YA KUPATA BOYFRIEND/MUME MWENYE MAISHA MAZURI……

The most awaited article is here!!! Lol….

 

Kwanza kabisa naomba uamini kuwa dreams do come true…. Yes unaweza ku end na yule unaemtaka wewe. Ila sasa tujaribu kuwa real kidogo kuwa chances za wewe kumnasa Brad Pitt and the like are close to zero…lol… So hata dreams zako basi ziwe na reality kidogo. Maana kama unadream kunmnasa BILL GATES chances are you will be disappointed.

 

Hapa mie ntakupa hints za kumnasa mwanaume mwenye maisha mazuri, sio tajiiiriiii ila mwenye maisha mazuri, ten asana tu. Ila kama you are lucky unaweza kumnasa BILL GATES wako kwa ushauri huu huu… Ila ndo hivyo tena mambo ya nyota. Hahahahhaha…

USHAURI WA KWANZA KABISA WA KUPATA MUME/BOYFRIEND UNAEMTAKA WEWE NI PRAYER…. NEVER UNDERESTIMATE THE POWER OF PRAYER…. SALI, LIA NA MUNGU NA ATAKULETEA YULE UNAEMTAKA, KAMA HATOKULETEA YULE UNAEMTAKA BASI ATAKULEEA YULE ANAEONA ANAKUFAA… MUNGU NI MWEMA NA SOMETIMES HUWA ANA NEGOTIATE. UKIONA ALIEKULETEA ANAKUFAA ILA SIO YULE UNAMTAKA PIA UNAWEZA  KUMUOMBA KWA NJIA YA SALA AMTOE KWENYE MAISHA YAKO AKULETEE YULE UNAEMTAKA WEWE….LOL….

 

Haya ngoja tuanze. Kwanza kabisa ujue kwamba jinsi ulivyojiweka,marafiki ulionao, sehemu unapoishi ,sehemu unazopenda kutembelea ndio haswa vitu vinavyo ashiria utapata mume/boyfriend wa aina gani. Kama ujuavyo mara nyingi mwanaume unakutakana nae either kwa kuwa introduced by friends, au ukiwa outing, au harusini, au kazini. I think wengi wamekutana na watu wao through introductions za marafiki. Sasa kama marafiki zako woooooooote ni wachovu ujue kuwa yoyote watakae kuintroduce kwako chances are nae ni mchovu. Ila kama angalau pia unajua na watu wenye maisha mazuri siku wakiku introduce kwa mtu, chances are huyo mtu anazo. Au vipi??? Pia kama unaishi kwa mtogole what are the chances that utaolewa na mkaka wa masaki? angalau jisogeze uishi hata Victoria, au Mikocheni.  Imagine mwanaume amekupenda alikuona Hyatt kwenye brunch haya ikaja firstdate , anakwambia ntakuja kuku pick up nipe address. Ooh mie naishi kwa mtogole.. hahahaha Kaka wa watu alete benzi lake kwa mtogole…. hiyo ni goodbye!

 

Tukija kwenye jinsi unavyoishi maisha yako, unapo hangout na unapoishi ntatumia mfano wangu mwenyewe. Nilipotuaga tu Dubai nilikuwa nakaa uswekeni panaitwa Deira. Tena kwenye apartment ya kushare watu kama 10. Kumbuka nilikuwa nimeenda kwenye interview hata kazi bado nilikuwa sijapata. Ila nilikuwa mjanja siku quit kabisa kazi yangu Stanbic Bank. Nilichofanya ni kuwaambiwa kuwa nahitaji kusafiri for a few days only ili kama kikinuka Dubai nirudi zangu kazini fastaaa….lol….. Bahati nzuri nikapata kazi a week later. Ila kumbuka bado nilikuwa nakaa uswekeni a.k.a Deira. Yani nilikuwa nadata hao wanaume naokutana nao nikisema hata niende dukani. Kiruuu yani ni wanaigeria tuuuuuuuu, ‘HOW ARE YOU MY SISTER”, WHAT’S YOUR NAME MY SISTER” .Sasa hiyo reaction yangu mngecheka mpaka mkae chini, jamani nilikuwa nanunaaaaa utasema huyo kaka aliwahi kunikosea kumbe ni kwamba tu nna hasira nasalimiwa na wachovu tu kutwa nzima. Basi nikisema nimuulize unafanya kazi gani Dubai, wote jibu ni lile lile “ I’M IN CARGO BUSINESS” Yani wanaigeria woooote wa Deira ni “CARGO BUSINESS””… Yani mtu alikuwa akinijibu cargo business basi navyobadilika sura na kuwa mkali ghafla utasema nna mood disorder…hahahahhaha Yani nilisema bora niwe single kuliko kudate huu uchafu… Ehh kwanza TZ nimeacha better guys alafu nije Dubai kukimbizana na hawa ma cargo business wa kinigeria , I’m sole chief…..

Ila umeona tatizo liko wapi??? Tatizo sio hao wanaigeria wala maskini ya Mungu? Tatizo ni langu mimi. Why am I putting myself in a position where these kind of guys can even have access to me??? So tatizo ni kwamba nilikuwa naishi in the wrong area. Huyo dream guy wangu ningempatia Deira kweli? Hapo Baba Kenzo anaishi Dubai Marina ukumbuke eeh? Mie niko Deira what are the chances our paths will ever cross? None. Haya angalia upande mwingine humo kwenye apartment naishia na wadada wa kiwest Africa, wengine wana vikazi vya ofisini wengine nilihisi ni machangu though sikuwahi kuwaona na wanaume pale sababu ilikuwa marufuku kuleta mwanaume kwenye ile apartment.Sasa kumbuka hao ndo shoga zangu wa Dubai. What are he chances kuwa through them ningemeet mwanaume wa maana? NONE right???

Yani niliishia kula vyakula vya kinigeria kutwaaa. Ila mpare nilikuwa nimeweka akili kumkichwa nasubiri tu nipokee mshahara wa kwanza nifanye mambo…. Hahahahahhaha…. Basi nilivyopokea tu mshahara wa kwanza nikahama DEIRAAAAAAAAAAAAAAAA…… Guess nilihamia wapi?? nilihamia JUMEIRAH BEACH, one of the poshiest neighborhoods in DUBAI. Only rich people live there. Yani hata ukitoka nje kwako magari ya barabarani yanayopita unaweza kushiba kwa kuyaangalia tu, maana ni noma. Tena nikitoka nje kwangu naona Burj Al Arab ile paleeeee….. Aisee Im not joking… Sasa je how did I afford to live where the millionares live? Nilipata sharing housing…. Yes, dubai kuna nyumba za kushare. Basi tulichukua mansion la vyumba 12 on JUMERAH BEACH ROAD. Kila chumba mnakaa 2 girls. Yes I had a room mate ,omg I loved that girl, Alikuwa anaitwa Sanaa mmorocco. So why go through all that? Well first of all I knew mwanaume yoyote ntakaekutana nae maeneo ya nyumbani kwangu akanipa hie he wont be a loser…lol… Sasa basi how much was this life style costing me? Well, let just say 80% of my mshahara was going into accommodation,yes hiko kichumba tu ,tena cha kushare na mtu, just because kiko in a mansion in Jumerah Beach. 20% into kupanda mabasi kwenda kazini, kula chakula, na kuvaa vigauni vya forever 21.Yani nilikuwa sisevu hata shingi moja.  Ila haikunipa shida coz I knew what I wanted…. Yes nilikuwa napanda basi kwenda kazini maana sikuwa na gari nilivyofika. Na mabasi ya wenzetu sio kama bongo kugombania na kulowa jasho. Kule full kipupwe tena hata bus stop mnasimama kwenye kibanda kina AC ndo msubiri basi. So although nilikuwa namaliza pesa zote kulipia hiyo room inside that mansion ila sasa viwanja vyoooooote vya maana vilikuwa ni either walking distance au ni taxi ride ya pesa ndogo sana . Wakati nipo Deira nilikuwa siwazi hata kwenda hivi viwanja manaa sina gari nikiwaza hiyo pesa ya taxi ya kwenda huko na kurudi ni balaaa. Either sasa nimchekee mnaigeria ani drive huko viwanja vya maana ila sasa ndo nikifika huko anigande, hahahahhaha nkawa naona bora nilale ndani tu na niwe single kuliko kuwa na mtu asie na msaada kwangu….

 

The mansion we were renting on Jumeraih Beach Road…… Invest in your future ladies…lol….

Basi nilivyohamia Jumerah Beach ndo nikaanza ku enjoy Dubai life,, yani kwanza nikitoka nje kwangu tu yale magari yanayopita Jumeirah beach road mie mwenywe tu najihisi nisha make it… ahahhahahahaha…… Alafu kule black skin unahesabu, nkasema hapa kweli lazma nipate my mzungu mume…. Hahahaha…

Basi kila siku nikawa ni outing, sehemu za maana tu. No low class clubs and bars, nope…. My room mate nae alikuwa single lady. Yeye alikuwa anafanya kazi another company,mie nilikuwa Barclays nilikuwa ki banking officer tu nothing much but it paid the bills. Ndo tulikuwa tunatoka outing wote…. She eventually married a local guy kama mke wa pili. Ila huyu kutoka nae ilikuwa shida  kweli maana yeye alikuwa anataka twende kwenye shisha tuuu maana huko ndo kwenye arab guys…hahahahaha

 

Ukiwa single and want to meet someone. Hang out kwenye viwanja unavyodhani utakutana na mtu unaemtaka wewe. Na isiwe unaenda mara moja kwa mwezi alafu siku zingine unaenda kwenye viwanja vyako vya uswekeni. NOPE.Change your lifestyle completely. Acha kwenda ushuzini. Nenda huko viwanja vya wenye pesa kila unapotoka. Yani hayo ndo yawe maisha yako. Hapo kweli utakuwa na chance ya kukutana na mtu….. Hata kama you cant afford them we nenda. Kanunue fanta orange yako moja unailamba lamba the whole night. Ila sasa sio upewe offer uagize bia. Nope . Be classy. Hata ukipewa offer endelea kunywa fanta yako.  Also achana na night clubs. Very few hardworking men with good money go clubbing. They work too hard during the day to have any energy to go clubbing. Go to lunch, brunch, dinner bila kusahau Lounges and very classy upscale bars. Achana na clubbing. Kuhusu kwenda wrong places, ndo maana watz wengi walioko nje lazma waolewe na watz wenzao au na wanaume wasio na kitu sababu ya hangout, mtu uko ulaya/marekani ila kutwa kufatana matakoni na watz wenzako hivi utapata mwanaume mwingine zaidi ya mwanaume wa kitz? akitoka outing basi ni kwenye function za wabongo tu, sijui harusi, sijui Khadija Kopa kaja, sijui Mzee Yusuf kaja, akienda club basi ni club za watz au akiwa na class basi ni aende club za wanaigeria…hahahha…Hivi huko utakutana na mwanaume wa maana kweli? sana sana ukutane na likaka halina hata papers  na kazi za kubeba box na bado linakucheat. maana huku wadada kwa kuchukuliana mabwana ndo maisha yao. Sasa hao wanaume wenyewe wanaowaendesha ni kituko tu maana shingi tano hawana.lol…Kitu kingine ni kwamba NEVER GO OUT BY YOURSELF,NEVER EVER. Only prostitutes go out on their own and seat at the bar all alone. Yani ukishaenda out peke yako unaonekana changu tu hata kama sio changu. So utakuwa approached na mwanaume ambae anataka kukulala tu akupe vijihela asepe zake. And that’s not what you want. You want to meet someone ambae atakuja kuwa mumeo so jiweke kiheshima. Na mnapokuwa out sio mue macho juu, mnapepesa macho kutizama watu. Mtastukiwa fasta…. Relax, enjoy yourself, yani muonekanae mko pale ku enjoy sio kutafuta mume. Hahahahahhahahahahahahha….

 

Okay, so back to my story. Basi katika toka toka zangu zile za viwanja vya maana, one day nikawa introduced to the HUMAN RESOURCES DIRECTOR OF DUBAI WORLD. Yes Dubai world, which is the biggest company in UAE. Chezea mpare hapo hapo nikachomeka kuwa natafuta another job coz the current one siipendi. Uwiii 2 weeks later I was working at Limitless – which is one of Dubai World’s subsidiaries and guess who else was working as a consultant at Limitless??? Baba Kenzo…… Ila hatukukutana ofisini ingawa tulikuwa tunafanya kazi hapo hapo…. Kulikuwa na another employee wa hapo hapo Limitess, a very very big boss ambae pia alikuwa married akawa na kaji crush na mie, ila sikuwa interested at all maana mie at that time nilikuwa natafuta mtu serious na sio mume wa mtu wa kunipotezea muda wangu. Ningekuwa natafuta buzi labda ,ila nilikuwa nataka mtu serious. So familia yake ikawa imeenda Australia for X’MAS yeye akawa kabaki Dubai , akaniaomba niende nae out for drinks on new yr’s Eve. Nikamwmabia the only way I will go is if aalike wanaume wengine na mie nialike other girls ila just 2 of us hapana….Akasema poa. You know why nilimwambia afanye hivyo? maana the guys alikuwa one of the big kahuna’s wa Dubai World ,obviously marafiki zake watakuwa wakaka wenye maisha yao mazuri. So guess who he brought ????? he brought Baba Kenzo and his cousin sister na mie nikaenda na rafiki yangu. Basi mie na baba Kenzo we hit it off hapo hapo and the rest is history…. Huyo baba anamtaniaga Lance mpaka leo ,anasemaga wewe nimekualika ukanisindikize mimi alafu umefika ukanipiku… hahahahahhaha….

What I wore the very first time I saw Baba KENZO.

The very first time, I met baba Kenzo…. DEC 31 2007. Baba Kenzo and were so sad Burton alivyoshindwa kuja kwenye harusi yetu sababu yeye ndo alietu introduce. Baada ya kumwambia asije mwenywe aje na friends na mie nije na friends basi akaniletea baba Kenzo….

So that’s thats where i learnt  kuwa baba KENZO nae alikuwa hapo hapo ofisini kwetu. The company was too big , theres no way unaweza kumjua kila mtu. Ila kila mwanamke single alikuwa anawavizia sana maconsultant wa kimarekani na ki British coz walikuwa wanakula bara refu maana mwarabu anavyomwabudu mzungu. Yani waarabu wa Dubai jamani sikuwaelewa wanaowana wazungu kama Mungu.. Yani walikuwa wanaishi kama kings……

 

So what can be learnt here? Hang out sehemu za maana tuuu au sehemu ambazo unajua wana hang out wanaume unaowataka wewe. Hata kama hutopaa boyfriend/mume hapo u will meet wenye nazo ambao mtajenga urafiki na watakusaidia sana hata kama sio kipesa. Kama mie huyo Director wa HR nilie mmeet. Yani wala hakuwa na interest yoyote ya kimapenzi na mimi and vice versa maana alikuwa na familia yake Ila ndo tukawa marafiki na akanisaidia kupata bonge la kazi. Yani mshahara wangu ulikuwa tripled na huko huko nikapata mume. So its NOT all about kupata mwanaume  ila pia kuwa friends na watu wa maana watakaoweza kukusaidia au kuku introduce kwa watu wa maana kama wao……

 

Anothet tip nawapeni ni kwamba achenI kuomba hela. Hata kama wewe ni maskini una matatizo usiombe pesa. Nothing drives away a man faster than mwanamke anaeomba pesa from the get go. When I met baba Kenzo nilikuwa nalipa bill half half mpaka siku nilipochoka na kumwambia nimeshindwa biashara ya half half. Mtu analipwa mshahara mara 20 ya mashahara wangu na bado nalipishwa half half… Ila sikufanya fastaa , hapana nilisubiria kasha fall deep in love  ndo nikaanza kuonyesha uafrica wangu wa kukataa kulipishwa vitu nakutaka kuwa spoiled…. Hahahahahhahahaha… So uwe na subra ,especially na wanaume wa kizungu hawajui kuhonga ila they can learn. Hahahahha… MFUNDISHE TARATIBU Ila sio date ya kwanza tu unaanza oooh mdogo wangu anahitaji school fees, mama anaumwa figo inahitajika pesa ya hospital, hutomwona. Mwache kwanza anogewe na wewe ndo uonyeshe jinsi ulivyo omba omba…… Ila baba Kenzo alinitesa mwanzoni jamani. Mtu ananipeleka expensive dinners alafu napewa bill yangu. Yani diet ilizidi mara kumi ,full kula starter tu alafu najifanya nimeshiba. Ahhahahaha, alivyoanza kulipa bill nzima nilianzaje kuorder ma rib eye steak ???? hahahahahhaha……..

 

Another tip ni kwamba harusini pia watu wengi huwa wana meet watu. So jaribu kwenda kwenye harusi za maana…hahahahha. HARUSINI watu wengi huwa wako kwenye mood ya mapenzi hata wanaume nao. Ila sio uende wedding za uswekeni nenda za maana…….

 

Kuhusu kuvaa, vaa vizuri. Decent man want decent looking women. Sio utoke out mtu hawezi kutofautisha kati yako wewe na changu. Lazma mwanaume akuangalie na ajue Yule pale nae mfata sio changu. First impressions matter. That being said ,it doesn’t mean utoke looking like your mom.HAPANA. All men love sexy women, na looks ndo huwa zinavutia wanaume. So vaa nguo zinazoonyesha uzuri wako, look sexy. A little bit of cleavage sio mbaya. Nachosema ni kwamba usiwe nusu uchi na pia usivae kama unaenda kanisani. Yani tafuta balance hapo kati kati…….

 

Ukiacha hiyo njia ya kukutana na mtu face to face. The easiest way to have a million dates without looking like a whore au without kumaliza viwanja vyote mjini ni online dating… Trust me so many people now meet others online. Yani najuana na watu kibaooooo who have met their hubbies online. Tena kwa wale mnaotaka wazungu this is the 100% sure way kuwa utapata mzungu. Yani hii nia haina longo longo. Hapa lazma umnase mzungu ila sasa inabidi uwe makini upate mwenye maisha mazuri. Maana wengine waongo atakwambia ana hiki na kile, akutoe Tanzania ufike maulaya umkute kwenye welfare. Au wengine wauwaji anataka akuoe ili akukatie life insurance akuue achukue mamilioni yake….. Ofcourse sijawahi kusikia mtu aliepatwa na kitu kama hiko ila ni katika kuchukua tahadhari tu.

Never ever use free dating websites. All weirdos wako huko. Utakutana na uchafu wooote kwenye free websites. Ili uwe successful be as honest as you can be. Sio uweke picha yako ya miaka 50 iliyopita wakati una 50kgs alafu siku mtu anakuona live una kilo 100. Atakukimbia. Weka picha zinazoonyesha jinsi ulivyo kiuhalisi. Picha 5 hivi ndo zinatosha.Tumia jina feki tu kwenye website. Baadae utampa jina lako la kweli. Uwiii utakutana na wanaume elfu 5 kidogo ila sasa kuchagua kati ya hao elfu 5 yupo bora ndo kasheshe… Alafu sasa huwezi amini wanaume wenye kazi za maana na pesa za maana ndo wanatumia sana hizi dating website sababu hawana muda wa kwenda out kumeet watu na kudate. Na wengi tu wanataka ku meet mtu serious asettle down sababu yuko very busy hana time ya kupoteza kudate wanawake 500. The website ambayo karibia kila mtu anapata success ni WWW.MATCH.COM . Hii site ni expensive kidogo ila its worth every penny. Yani unaweza hata jifungia ndani usitoke ili uwe unachat tuuu….lol.. Unaweza kusaka wanaume wa nchi zote Duniani. 

Ina cost $40 per month. Sio mbaya  kama una invest kwenye future yako. Kuna mtu namjua alikutana na millionare kwenye hii website.

 

Anyays kwa vile mpare napenda pesa ntawasaidia wale ambao hawana credit card . Ina cost $40 per month mie ntaku charge $60 per month kwa matumizi ya credit card yangu. Kila mwisho wa mwezi unanikumbusha unanipa password na username yako naingia nakufanyia payment unaendelea kuhunt….hahahha

Nikiwapateni watu 100 tu uwiii naingiza kidola $2,000 kila mwezi kwa raha zangu….hahahahhaha…….. Kuna cheaper dating websites ila hi indo the best in the whole world…. Yani ndani ya 6 months kama hujapata mchumba basi shoga una gundu ukamuone Shekhe Yahya tu akuoshe nyota…..lol……

Kama huna credit card na unataka nnikusaidie kulipa kila mwezi  kwa card yangu nicheki kwa whatsapp +1 305 498 3696. Au email mangekimambi@hotmail.com. Naweza kuchelewa kidogo kujibu maana nna ma meseji mpaka basi ila ntajibu soon as I can.

Last tip ukipata mtu mkapendana ,akaja TZ kukuona mkapendana hata zaidi mkaamua uhamie alipo. Instead of processing a fiance Visa au sijui aje TZ akuoe then uombe spouse visa omba kwanza visit visa. Jifanye unataka uende tembea tu alafu ukifika huko ndo unawachenjia kibao kuwa hurudi unataka visa ya mke. Maana hizi spouse visa kwa relationship za online uwiii utawekwa TZ hata 2 yrs unasubiria  visa mpaka mwisho jamaa achange his mind bure.Lol. So try other visa’s kabla ya hizo za uhamiaji…. Mie nilikuwa nna ndoa ya 3 yrs  na mtoto juu na bado nilikalishwa tz 8 months kusubiria visa mpaka Kenzo akaanza kumsahau babake. Na hapo watu waliniambia nimeipata mapema. Sasa wewe wa kukutana na jamaa online utapiga 2 yrs bongo kusubiria visa.

PS: Uwiii jamani hii article mbona ntawakoma haters  sasa??? hahahahhaha ntasemwajwe nawafundisha kugold dig…..hahahah…. Ntatukanwaaaaa uwiiiiiiii….hahahhahaha

Read More

X’MAS TINGZ WITH FAMILY……

I removed the weave a few days ago. Yani sikukaa nalo hata wiki…

uwiiii mpare nikiwaza $250 yangu niliyolipa kusukwa lile weaving nadataaaaa….

Yani kusema ukweli weaving zimenishinda jamani….

Im slowly learning to love my own hair……

Make up by me….lol…

Stepping up my makeup game….Ignore the eye lashes bado sijajua kuzibandika vizuri..This is the second attempt ya kujipaka eye shadow… Yani nilikuwa sijui kabisaaaaa….

Thanks to youtube video and thousands of dollars worth of brushes and products ,im finally learning…. I think i went over board wakati nanunua

products za kujifunzia makeup vingine sijui hata kama ntakaa nivitumie. Yani nikiangalia video mtu aki mention kitu alichotumia kama sina nipe dakika 5 nishazama online kuninunua….lol….

Ukiamua kukaa na natural hair inabidi ujifunze kupaka makeup maana kuwa natural hair alafu bila makeup utakuwa kaa housegirl….hahahahahha

Mama watatu…..

Baby ake mami huyuuu…

#firstborn #myfirstlove

hahahahaha…. love this baby….. mwaaah…

kesho kanasafiri kanaenda London kwa babake, ntakamisijeeeee uwiiiiiiiiiiiiiiiii……

Tutakuwa tunapeana zamu kula nae X’mas. Mwaka jana na mommy, this yr na daddy… Ila nahisi naanza kudata already…uwiiii….

Ndo shogangu huyu mwenyewe…

MAMA YAO KINA NANI HUYU?????

uwiii bado najifunza kupaka make ila duh nimejua ku contour pua yangu, inakuwaje straight kama ya msomali…hahahhaha

poser…

Muke ya Muzungu……..

Bhoke, jamani mtoto kawa mrefu mpaka naogopa….eti kameanza kunipita urefu….

Mommy and Keanu

Uwiii daddy karudi leo,, basi kufika tu akambeba KENZO wake wakaenda park. Mie nikawababe wanangu Bhoke na Keanu. Tukasema twende zetu  Farmers market tukale  Brazillian nyama choma . Mara Kenzo na babake hao wametufata…

Hapo wamesimama kwenye foleni ya nyama choma….. uwiii watu wanapenda hii nyama yani sijawahi kwenda nkakuta hakuna foleni….

Hivi mmemuona Bhoke alivyokuwa mrefu jamani… eti anataka mfikia hata Lance…huyu mtoto jamani…

Kanaingiza thirteen in January.

Make up by me…. uwiii soon i will b doing makeup like a professional jamani…. hahahhaha…

Baada ya kula nyama choma tukaenda kuangalia X’mas show at the Grove….

chezea KEANU na yeye yupo busy…

My people…

Ndo karudi leo, full kudeka…. hahaha…

Hivi did Baba Kenzo pull a Kanye West on me? mie namkiss yeye mikoni mifukoni? lol

hilo smile lake….lol…

AWWWW…

Mwanangu Bhoke jamani akishika camera ni balaaaa, haachi kupiga picha….

The X’mas show was awesome….

Keanu and daddy….

Keanu and daddy ake….

Keanu,mommy and daddy

hahaha Bhoke huyo, hata nikitembea picha…lol..

hahahahha ,,,,

mapenzi niueeeeee!!!!

Chezea kumisimiana ,full mapenzi ya kihindi…. hahahahaha

sasa mwoneni Kenzo anavyojiliza eti hataki babake anibebe mimi, eti ambebe yeye…

hahahaha

Jamani Kenzo ana wivu na babake.. Eti kakaa chini analia kabisa kama kapigwa kisa nimebebwa na daddy ake yeye…

Tusiokuwa na baba tutakoma…

Haya na yeye akabebwa…muone anavyofurahi…hahahahaha

Too much love for daddy today… we missed him so much…

Huyu cute baby wa nani????

Me and my bestie…….. (Im her mom first, then her bff,lol)

Kenzo and mommy…

I must frame this pic…

Kenzo throwing a coin into the fountain and making a wish…. awww

Flawless makeup by me….. My makeup game is getting really strong….lol…

Jamani leo mume wangu kanisifia nimependeza mpaka basi. Kasema akiniona tena na yale manywele ntakoma…

Kwa jinsi alivyonisifia leo naamini nikimwomba unyumba hatoninyima!!!! hahahahahaha

ZE END…..

HAPPY HOLIDAYS FRIENDS

Read More

DIAMOND ATANGAZA PENNY ALITOA MIMBA 2……..VERY SAD!!!!!

Jamani I have nothing against Dai… IM A HUGE FAN OF HIS WORK…. Kwangu hukosi kuskia nyimbo zake…..so napoongea sio chuki jamani ni kwamba tu hiki ni chombo cha habari…….

Hii interview dah, imenisikitisha mnoooooo, kwanini anaongea sasa huyu jamaaa? why tell people Penny alitoa mimba zake mbili? hivi anajua implication ya hiyo kitu kwenye maisha ya Penny? kwanza it’s illegal kutoa mimba in Tanzania. Pili Penny anatoka familia ya kiislam, ana kaka zake, mama yake na  ndugu zake. Kweli watamwangaliaje binti yao kujua alitoa mimba mbili za huyu jamaa? Acha hiyo tu , Penny bado ni mdogo anahitaji kuolewa hivi ni mwanaume gani atafurahi kujua mkewe alitoa mimba 2 za mtu mmoja tu??? Hivi huyu anajua jinsi wanawake wanavyoficha hiyo issue ya kutoa mimba? yani mtu hata uolewe ushindwe kuzaa au upate matatizo humwambii mumeo kuwa ulitoaga mimba. Kutoa mimba huwa ni siri ya mwanamke tena anakufa nayo mwenywe yeye na Dr aliemtoa mimba. Alafu yeye anamtangaza mtoto wa watu katoa mimbi, tena sio moja, mbili.  Yani kamtia yule mtoto doa kubwa mnooo. Na wale wanaomchambaga Penny huko instagram mbona ndo watapata cha kumchambia zaidi…..

Diamond ni mdhalilishaji mnoooooooooo wa wanawake… He doesnt think akiwa anaongea. DAH KABOA MNOOO… Hivi unaongeaje on TV kuwa gf wako alitoa mimba 2 tena unamtaja na jina? Huyu mtoto usupa star wake utakuja kuisha vibaya maana anaelekea pabaya saSA… Kusema ukweli mimi I thought wanaume wanaowapenda mama zao au waliO close na mama zao huwa wanadhamini sana wanawake ila huyu star weti kaonyesha kuwa sio wote…. Duh. Hivi Petitman siku akiongea on tv kuwa Esma alitoa mimba 2 yeye atajiskiaje? atafurahi kweli???? VERY SAD!!!!

Ila pia  mie kama naanza kumstukia huyu kakake Wema, analalamika Penny alitoa mimba zake, Wema alikataa kumzalia mtoto… yani na usupa staa wake woooote kweli hawa wanawake  woote wanakataa kumzalia? mie nahisi kama  kijana wetu is shooting blanks!!! lol (kama hujui kithungu google). Yani kwa jinsi alivyo na wanawake kila leo lazma mmoja angejibebesha  mimba hata kwa kuiba condom na kujidunga sindano za **** ili imradi apate mimba… Penny alivyokuwaga kafika kwa Diamond anasubiri ndoa kweli achomoe mimba mbili??? mweeeh??? mie naona kama anajitetea sana kuhusu swala la mimba? mdogo wangu Wema alivyokuwaga ready kufa juu ya Diamond na tayari kwa ndoa kweli akatae kuzaa nae? mmmmh!!!! asije tu baadae akasema na Zari nae alikataa kuzaa amzalishe tu hata kamoja, hahahahhahahaah…….Yani the biggest supastar in East Africa unapiganiwa na mademu kona zote alafu eti wanawake hawataki kuzaa nae wewe?? nani kaona hiyo???? yani by now Diamond alitakiwa awe na watoto wa kusingiziwa kama 10 hivi. lol… Hamuoni mwezie Ali Kiba  kidume cha mbegu, UK ana mtoto, sijui na mji gani naskia ana mtoto…Yani yeye akienda nchi za nje kwenye show lazma aache copy yake huko…hahahahhahahahha

 

 

2yrS ago kwenye hii interview alisema Wema ndo alimpiga msasa wa english, leo kawa Penny alafu anasema watu huwa wanadhani Wema ndo kamfundisha english, hakuna mtu aliedhani Wema ndo kamfundisha english yeye mwenyewe ndo alietuambiwa kuwa Wema kamfundisha….. Cheki kuanzia dakika ya 14……

uwiii, goodnight saa kumi usiku, ngoja nikale nimekalia umbea tu kisa sina wa kulala nae. BRING BACK BABA KENZO……LOL

 

 

Read More
1 2 3 128
Designed by muzemultimedia web design Tanzania