MASKINI CHIDI BENZ………….

Tanzania bwana, basi hapo polisi watampelekesha Chidi weeeee, huku the real culprits wanakula bata tu…

Jamani Chidi is a victim of unga. Amekutwa na unga una dhamani ya tsh 38,000, which means ulikuwa ni unga wa personal use sio wa kumuuzia mtu.

Sasa huyu ni victim ana anahitaji msaada na sio kufanywa kama jambazi… Yani bongo hopeless sana. Badala wa deal na chanzo eti wanadeal na kina Chidi…

Ingea pande hizi huyo kwanza angepewa dili kwamba ataje nani kamuuzia then yeye apewe kiji probation, especially coz ni kosa la kwanza….. 

Ila bongo hawana hata time ya kumpa Chidi dili kama hili ili awape source ya hayo madawa wao busy tu kudili na Chidi na wakati mtu ni mtumiaji… Anatakiwa kusaidiwa apone aachane nayo na awataje wanaomuuziaga ili yeye aachiwe huru……..

Ndio kusnitch sio poa ila kuliko ufungwe si bora u snitch tu…..Huku mtu akiona anaenda jela ana snitch fastaaa tu….

Pole Chidi ,tuko pamoja,ukitoka please nenda RAY C FOUNDATION usaidiwe upone……..

Ila kakangu huyu nae jamani sijui ndo alikuwa high akasahau anaenda panda ndege na sio basi, akasahau zile security za airport…..

Read More

U-TURN’S 37 DAY WEIGHT LOSS CHALLENGE – DAY 14……..

Weight  niliyoanzia nayo hiyo….. 67.5kg

Hii ndo weigjt yangu ya siku ya 7…..

Hii ndo weight yangu ya leo, siku ya 14………

So nimepungua 2.4kgs this week… This is really good….. Wiki ya kwanza ndo wiki ambayo unapungua kwa kasi mnoooo

sababu most of the weight inayotoka sio mafuta bali ni maji… ila hii wiki iliyoisha ndo haswaaa tumekuwa tukipungua mafuta na sio maji tena…..

 hii ya tatu pia tu expect kupungua kilo 1.5 -2.

kama hujapungua 1.5kgs  au zaidi wiki iliyokwishi wewe unacheat mnoooo….

Sorry last week sijaweka post yoyote ya diet…This week ntaweka more postS za diet…..

Haya challenges ni zipi????? Mie biggest challenge ni kwamba Baba watoto is in town, sasa anataka twende dinner, sijui drinks..Duh.

Ila namtoleaje nje, i feel bad maana atarudi tena kazini, ila kutoka kwa kweli kwa sas siwezi kwanza sina nguvu, pili nikitoka lazma ntakula tu akiagiza kitu,,,kanunajeeeee,,, ila angalau during the week he is super busy na mikutano yao mpaka usiku……weekend ndo balaaa…..lol…

Sasa hivi sitamani tena vyakula vya wanangu sijui ndo mwili unaanza kuzoea, au ni vipi, ila uroho kama umepungua mnoooo, hata njaa sio kali vileeee kama mwanzo. Ehhhe niambie na nyie wapenzi wangu, mnaendeleaje na diet…

Mmepungua kiasi gani?

Read More

SITTI MTEVU ATAONA RANGI ZOTE MWAKA HUU……

Haya ma form ya immigration ya marekani yametolewa yakionyesha age ya bidada……

Mdogo wangu Sitti ,nilikushauri 2 weeks ago jinsi ya kuvua hili taji bila kupoteza utu wako,au heshma yako, ila hukusikia…

Next time jaribu kusikiliza  dada zako… Sasa hivi hata uvue taji yani umeshapoteza utu wako,heshma yako na ya familia yako na ya Miss Tanzania as a whole…  

Hhahha DJ Choka ni kiboko….hahahahahhahaha

Nakushauri kwa mara ya mwisho, vua hilo taji mwenyewe uendelee na maisha ya uraia wa kawaida kama sisi wengie, la sivyo hii issue yako itafika mbali mnooooooooo…… Watu wamekupania mnoooo, alafu bora kama ingekuwa wamekupania alafu wewe hujacheat,ila ume commit a fellony,haya mambo yatakuwa mabaya huko mbele, mbaya zaidi hutoanguka wewe peke yako, wataanguka watu wengi mnoooooo kuanzia hao waliokupa vyeti vipya mpaka baba yako ambae ni mbunge na amekaa kimya anaku support kudanganya wananchi… Unaharibu career ya babako sababu ya crown ya Miss TZ? WE demu kiboko aiseeeee…..

Wananchi wameamua hawakutaki sababu umewadanganya sasa kwanini unawa force? Miss Tanzania inabidi ufanye kazi za jamii sasa utafanya kazi ya jamii ipi kama wanajamii wanataka kukupiga mawe???????

PS: Swala la Sitti kuwa na mtoto jamani ni uongo 100% , ila kuna comment moja ilinichekesha huko insta yani niliecheka hadi mbavu ziliuma. Mtu alisema ” Huyu Sitti asipovua hilo taji tutaleta mpaka picha akiwa anamnyonyesha mwanae” Kha…..

Read More

MUUZA MADAWA YAKULEVYA WA MAGOMENI ADAKWA…….

UWIIIII HAYA CHONJI AMBAE NI MUUZA MADAWA MAARUFU WA MAGOMENI

AMEDAKWA LIVE LIVE NA MADAWA YAKE NA POLISI NA SASA YUKO NDANI. YANI HUYU HATOKI TENA…

UWIIIII SASA POLISI WAMEFIKA MAGOMENI……..

UWIIII WALIOOLEWA NA MA DRUG DEALERS WA MAGOMENI MATUMBO JOTO SAA HIZI… HAHAHAHAHHAHA

UWIIII TENA BESTI WA MUMEO NDO KAWEKWA NDANI, UWIIII NAHISI MUNAKUWA HAMLALI USIKU MNASIKILIZIA GETINI KAMA POLISI WAMEFIKA…HAHAHHHAHAHAA

UWIIIIIII , JAMANI KUNA SIKU WATU WATAKUJA SEMA KUMBE MANGE ALIKUWA ANASEMA KWELI,,,HAAHAHAHAHA

HAYA YETU MACHO……

ACHA SIE TUUZE VINGUO TUPATE VIHELA VYETU HALALI, NA WAUME ZETU WAPINDE MIGONGO KWENYE OFISI ZA WATU WAPATE VISENTI VYA KULISHA FAMILIA……

WANAOPENDA MTEREMKO NA MAISHA WASIOYAWEZA MPAKA WANAUZA MADAWA YA KULEVYA AU KUOLEWA NA WANAOUZA MADAWA YA KULEVYA KUNA SIKU WATAONA RANGI ZOTEEE………

JAMANI MSHAONA MAMBO YAMEHARIBIKA WATAFUTIENI WAUME ZETU KAZI ZINGINE JAMANI HATA KAMA IT MEANS KWAMBA MKAISHI

MBAGALA, SI BORA MKAISHI MBAGALA ILA USIKU MNALALA KWA RAHA BILA WASIWASI KULIKO KUTAKA KUISHI KWENYE MAGOROFA HUKU ROHO JUU JUU…..

HAYA NGOJENI SASA SIKU MTOKE FROM MAGOROFA TO SEGEREA TO MTAMJUA NZOWA….

SIMOOOOOOOOOOOOOO

KWA HABARI ZAIDI DUMBUKIA HUMU……

 

UPDATEEEEEE:::::

Hahhahaha hii story imewagusa wasomaji wangu huko, maana

inside informationa zinamwagika kwenye what’sapp yangu

Niliona comment jana usiku mtu kaweka akielezea mkasa huu ulipoanzia na yeye alisema kitu very similar na hiki,

ila kumbe its even worse hawakumpiga , walimteka then vijana wakambaka mtoto wa watu. Nilitaka kushangaa kupigwa tu ndo

wazazi wafatatilie kesi mpaka huko juu kumbe walimbaka bwana… Duh imagine umelea mtoto wa kiume ,lijali hajui ushoga wala nini

leo mtu atume watu wambake mwanao kisa madaya ya kulevya,duh ningeua mtu……

Haya kila mtu anataka kuwa top in town kama Khadija Kopa kwa njia yoyote ile…. hahahahahhahahah

Read More

HOLLYWOODSHOPAHOLICS KUUZA KUPITIA MTANDAO TU…. #ONLINESHOPPINGFORTZ

Leo haikuwa siku nzuri sana kati yangu na wateja wangu….. Baada ya mimi kuamua kubadilisha biashara yangu…

Kwanza niliwaboa baada ya kuwaomba wawe wana comment kwa english, hata broken english ili tuweze kuwakaribisha na wateja wa mataifa mengine…

Nikawachefua zaidi baada ya kusema sitopokea tena malipo ya mpesa na kwamba kuanzia sasa ni mauzo ya kwenye website tu….

Aiseee, kwa kweli nimevumilia for 4 whole months ila nikaona things are just getting worse…

Jamani kuanzia around saa 4 asubuhi mpaka around 5pm all im doing is replying to silly whatsapp messages.

Yani tunafanya biashara kama hatujaenda shule, hapana aiseeeee…

Imagine mteja ana anatuma message kwenye whatsapp kuota order, then mie nitume message TZ wanichekie huyo mteja kama kweli kalipa, then  anaitwa nani, niwape jina

waconfirm, then ndo ni process order.  nikitaka kukumbuka hiyoorder niitafute hiyo chat ni scoll up.. uwiii ni shidaaaaa.. hapo bado nna message mia 5 kidogo watu wanauliza mambo ya kijinga kijinga, mtu anauliza “hivi hii nguo kwenye mwanga mkali rangi inakuwaje”, naaaah nimeone bora nichukue hiyo risk ya kupoteza wateja wangu  wengi niendelee na wateja wachache ambao wako tayari kujoin the rest of the world kutumia technolojia ya internet

hayo ya whatsapp chat na malipo ya mpesa ntawaachia mauzaji wengine

nimespend thousands of dollars kutengenezewa website aalafu siitumiii natumia message jamani, eti kisa watu wanaogopa tu kujaribisha online shopping….

Anyways, wateja wangu mlioenda shule naomba sisi tuwe mfano kwa Tanzania ,naamini baadae watatujoin tu…..

kwa sasa ukipenda chochote kile nachopost instagram huna haja ya kumuuliza mtu kitu ,wala kumtext mtu ,wewe ruka kwenye website tafuta unachokitaka nunua na ATM card yako basi.

Kama huna hujui kutumia internet au kununua kwenye website yetu usijali naomba uende kwenye ofisi zetu @ Dar Free Market

1st floor, shop #37. watakusaidia na kukufundisha jinsi ya kununua kwenye internet.

JE unapataje card ya kununua online?

waweza kwenda crdb bank, fungua account nao. Wana service yao inaitwa simbaking. Hii simbanking ina link simu yako ya mkononi na account yako ya mpesa na bank account yako. ukitaka nunua kitu kama account yako ya benki haina pesa huna haja ya kwenda bank kupanga mifoleni, ingia kwenye mpesa yako peleka pesa kwenye account yako ya ban huchajiwi hata senti moja.

make sure ukiwa unaomba atm card waambie unataka card ya kununua online ili waifungue……

ukishapata card kama hujui kununua nishasema nenda ofisini kwetu   na card yako wana computer nzuri ina internet  wakatakufundisha ili next time hutokuwa hata na haja ya  kwenda ofisini utaweza nunua mwenyewe….

Mapokezi ya vitu ni pale pale dukani, imagine kama inabidi nikupe refund nabinya kidude tu kwenye website pesa yako inarudi moja kwa moja kwenye account yako ya CRDB…..

Nawapenda sana  … kwa maelezo zaidi piga 0764 484700….

WWW.HOLLYWOODSHOPAHOLICS.COM

Read More
1 2 3 116
Designed by muzemultimedia web design Tanzania