MAONI YANGU JUU YA ALI KIBA’S NEW SONG – CHEKETUA…….

mmm

Aisee ngumuje kupata time ya kufanya biashara, kulea familia then kublogua???? Nakomajeee…

 Anyways,  leo nimepata chance  ya kusikiliza nyimbo mpya ya Ali Kiba fasta fasta….

I like Ali Kiba’s music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za zamani… Au labda tuseme yani  nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina tofauti.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo sana…… Nyimbo zake za zamani zilikuwaga nzuri sana , ila pia yawezekana za sasa hivi zinaoneka sio nzuri sababu zimefanana na za zamani…Yani nyimbo ya Ali Kiba hata uamshwe usingizini bila kusikia hata sauti ukisikia biti tu unajua nyimbo ya Ali Kiba….lol….

Kwenye issue ya kiwango cha nyimbo kushuka hayuko peke yake hata besti ake  Diamond pia nyimbo zake zimeanza kushuka kiwango…. Mie naona tatizo lipo hapa…. Ni kwamba wamesha maliza material zao zooooote  nzuri…. Ni sawa  na kwenye mashindano ya kukimbia unapoanza kukimbia unakimbiaje fastaaaaa kama gari vile, ila mwisho wa mashindano nguvu zinaisha unaweza hata anza tembea…Mie naona ndo kama hawa vijana, wameshaandika all the best stuff they have sasa material zimekwisha inabidi wafanye tu ili mradi watoe new single….

Yani kwa Ali Kiba kwa jinsi alivyo under pressure sababu ya hiyo ya likinganishwa na Diamond naona hii new single imemwangusha kabisa yani na sasa ni dhahiri kuwa yeye ni number 2. 

Well, kunapokuwa na tatizo lazma tutafute na suluhisho… Tumeshajua tatizo sasa hivi ni unandishi wa nyimbo sio kwamba hawajui kuimba kama zamani. Talent zao zipo pale pale au hata labda zimeongezeka kutokana na experience ila problem is hawana tena material ya kuandika nyimbo. I think hata VANESSA MDEE  na  JUMA JUX   wanaface   the same problem. Yani Vanessa na Juma Jux wana swaga za hatariiiiiiiii, yani wamekaa kimamtoni ile mbayaa ila tatizo ni nyimboooooooo, nyimbo hazina viwango vileeeee…..Well wafanyaje sasa???

I think hapa mie nimeona kuna fursa kubwa sana ya uandishi wa nyimbo Yes asilimia kubwa ya artists wengi wa marekani huwa wanaandikiwa nyimbo zao. Especially baada ya kuwa kwenye gemu for a while maana na wao huwa wana run out of material au aideas ndo hapo inabidi wanunue..

Kwa mfano one of the most popular hits in the world ule wa I will always Love you wa Whitney Houston – yeye aliununua tu,ule wimbo uliandikwa na mtu mwingine. I think uliandikwa na Dolly Parton. So kama Whitney angetaka sifa za kujifanya yeye anajua kuimba na kuandika songs zake mwenywe basi sidhani kama angejulikana dunia nzima kama alivyojulikana baada ya huo wimbo alioununua kwa Dolly Parton.  Au tuseme Michael Jackson, mnaikumbuka ile nyimbo yake ya Thriller wakati tuko watoto tulikuwa tunaipenda balaaaa, na ilikuwa number 1 hit all over the world. Guess what Michael Jackson hakuandika ule wimbo aliununua kwa mtu anaitwa Rod Temberton.

Yani kuna watu wanakuwa mamilionea kwa kuandikia waimbaji nyimbo. So jamani mie naona its time sasa watokeee professional song writters Tanzania waanze kuwaandikia hawa waimbaji wetu nyimbo. Kama sio hivyo ndo hivyo wataendelea kutoa nyimbo zisizo na viwango mpaka mwisho watasahauliwa maana kuna new artisits ambao wana nyimbo zao mbili tatu kaliiiiii watatoa tutawapenda then tutawasahau hawa.Kama wanataka kubaki on top of the game for many years inabidi waanze kununua nyimbo sasa.

Although kuwa song writter sio lazma wewe mwenywe ujue kuimba ila hawa waandishi wa nyimbo wengi wao na wao pia wanajua kuimba ila for some reason walishindwa kutoka so wakaamua watoke kwa njia ya kuandika nyimbo…. Yes, its unfair ila sometimes kuna nyimbo ukiimba wewe usiejulikana itaonekana mbaya ila akiimba Ali Kiba itakuwa number 1. so instead of kukosa vyote kama hujatoka wewe kama star kwanini usitoke kwa njia ya kuandika nyimbo ? kama ndo talent yako? Na wewe utakuwa star kama huyo anaeimba nyimba zako maana lazma aseme kuwa nyimbo ni ya kwako au kama vipi mlipane pesa ndefu sanaaaaa ili afiche kuwa kaandikiwa nyimbo which mie naona ni ujinga sababu kuandikiwa nyimbo sio kitu kibaya at all it only means you only want the very best hutaki kutoa nyimbo sizizo na viwango.

So wenye vipaji vya kuandika miziki anzeni kuandika muwape hawa watu maana yani wana full vipaji na video zao zimeenda shule ila sasa nyimbo zao zinawa let down ile mbaya…..

Kwa mfano VANESSA MDEE, natamani mtu amwandikie songi moja kali la R &B in english, uwiiiiii mbona atakuwa African sensation au hata world wide sensation over night.  Maana swaga zoooooote za kimamtoni anazo….

John Legend pia ni mwandishi kabla hajatoka alikuwaga anawaandikia mastaa nyimbo mpaka siku moja alipiamua asiuze nyimbo yake aimbe yeye mwenyewe ndo akatoka kama mwimbaji. 

Alafu kama mmenotice wasanii wa bongo hawatoi albums at all. Wanatoa single tuuuuu… Kama huyu ali kiba alivyofanya come back si alitakiwa atoke na bonge la album,instead akaja na single mbili. That again shows kuwa hakuwa na enough material kutengeneza 14 songs za kujaza album. Which shows kuwa waandishi wa nyimbo wanahitajika sana. Aisee its important for ana artist kutoa album jamani sio career yoote anatoa single tu. Our top artist Diamond ana album moja tu, how sad is that? Inasaidia hata show zako kunoga coz unakuwa na nyimbo mpya kibaaaa za kuimba. La sivyo kwenye show unaimba nyimbo mbili mpyaa zingine zooote za mwaka 2000. Again ntatoa mfano wa diamond, sijui kama wangapi wana CD ya ile album yake ya kwanza, uwiiiiiiii, jamani that album is crazy goood. Asikwambie mtu,jamani album ina nyimbo nzuriiii ile.  Uwii kuna nyimbo moja inaitwa kizaizai kwenye ile album uwiii naupendaje sasa???? So now Diamond akifanya show he has 2 new songs and the rest inabidi aimbe nyimbo za 4-5yrs ago sababu hajatoa album in a long time… Againa tunarudi pale pale sidhani kama ni kwamba hapendi kutoa album ila tatizo ni kupata nyimbo 14-18 za maana za kujaza album… So again, waandishi jitokezeni I think kazi zipo sanaa tu… HATA Ali Kiba nae ni same problem akifanya concert ni anaimba 3 new songs ambazo ni mbaya then the whole other time anaimba nyimbo zake zilizohit more than 5 yrs ago.Jamani nilienda conrcet ya Rihanna 2 yrs ago.. Uwiii,unajua mdada for 1 hour anaimba 1 new song after 1 new song, tena ndo nyimbo zinazihit at that time, mnakuwa mnazijua word by word, yani hapo kwenye concert nyimbo zoooote alizoimba ni zinahit all over the country hiyo ndo inaitwa tour. Sasa wabongo anasema anafanya tour huku ana 2 new songs nyimbo zingine zoooote za mwaka 47. Toeni albums jamani, lipeni watu waandikieni

Kwa kifupi na chosema ni kwamba kuna need kubwa ya song writters Tanzania. Na pia wasanii wetu ambao wameshajenga majina yao wasikubali kushuka kwa kung’ang’ana kuandika nyimbo zao wenyewe. Waaenze kutumia professional writters ili waendelee kubaki kwenye gemu…..

I swear nyimbo za Ali Kiba nimezichokaaaaaaaaaaaaa, nimezikinaiiiiiiiiii. YANI ZIPO VILE VILE ZOTEEEEEE…. Na Diamond nae asipoanza kununua nyimbo au kuandika very good songs  nyimbo zake zitaanza kuboa kama za Ali Kiba soon washangae vitoto vinakuja juu vinawafunika kwa kutoa great songs.

Read More

ETI MADAM KAENDA FANYA NINI SINGIDA????

Eti kidole cha ndoa cha madam kina nini vile????

Huko Singida madam na family yake wanasherehekea kitu gani ati????

Mie mwenyewe sijui ndo maana nauliza…..

Read More

JE UNAISHI BEIJING, SHANGHAI AU HONG KONG?????

Hi Wapenzi.

kama unaishi kati ya miji hii… NICHEKI PLEASE, AU KAMA UNAMJUA MTU ANAEISHI ONE OF THESE CITIES MSTUE PLS…NI MAMBO YA BIASHARA…..

PLEASE NTUMIE MESSAGE YA WHATSAPP

+1 305 498 3696

Read More

WEMA SEPETU – IN MY SHOES S02EP13

Nipo busy kidogo nikitafuta pesa… Embu burudikeni na mtoto Sepetu kwanza wakati nahenyeka…..

PS: Alafu mambo ya C’s mum mngeacha maana nachoka block comment… Jamani mbona yameshaisha…Ndugu wa baba mmoja tu huzozana itakuwa mie na C’mum…. Mbona kina KOKU wananiwekaga sawa nikikosea na tunaendelea na maisha???? C’S mum mtu wangu wa long time. Alafu si mnajua nilikuwa nna stress sana kikawaida nisingelipuka vile… Anyways, like I said freedom of speech ipo pale pale, kosoa mtu unavyojisikia ila tusivuke mipaka tu…..Ama nene!!!!

 

 

 

 

 

Read More

MAMBO YA ENTOURAGE – SWAGGA MPYA ZA DIAMOND

Naomba nianze kwa kusema kuwa Im not a hater….. Naandika kama blogger tu sio hater….

Ni maoni yangu tu kama Mtanzania na katika kumpa ushauri kijana wetu….

Anyways,wewe kama mtanzania unaonaje hizi swagga mpya za Diamona kusafiri au kufatwa nyuma na kundi la watu wakiwemo mameneja wake, ndugu,mpiga picha, etc….

Kwa maoni yangu naona kama mameneja wake wanampoteza tu. Itakuwa kaambiwa akitaka kuonekana ni big star basi lazma awe anafatwa nyuma na kundi la watu everywhere he goes.,,,,,

Nimemuelewa kidogo sababu labda kaona mastaa wakubwa wakubwa duniani huwa wanakuwaga na entourage kubwa ya watu ila jamani they can afford kuwa na watu wote wale… Some of them make over 10million dollars a year sasa kulipa watu wote hao kumfata fata ni pocket change kwake. Tayari wana utajiri ambao hata wajukuu zao watakuja kuukuta ,wana majumba in every city wengine mpaka Palm Jumeirah Dubai wana mavacation home sasa huyu kijana wetu ambae mpaka leo bado anaishi kwenye nyumba ya kupanga kwanini analipa watu kumfata fata nyuma hivi? wakati it’s very unnecessary.

Hvi whats the point of mameneja wake kumfata fata kila anaposafiri? Ndugu yake Romy Jones its okay kumfata fata, wata kuwa wanaenjoy ku hang out together all the time so anaona poa kumkatia ticket asafiri nae. Ila kwa uDJ mmmh? Hivi T.I alivyokujaga fiesta alikujaga na DJ wake?? labda mie mshamba sielewi…lol.. Aseme tu anaependa kusafiri na ndugu yake coz they are very close.

Madansa wake ndio wana ulazima ila hao wengine ni show off ambazo zinamrudisha nyuma….

WOOOOOTE TISA KUMI NI MPIGA PICHA ALIEMWAJIRI FULL TIME kumfata fata everywhere….

Uwiiiii, kweli only in bongo… Na huyo official photographer ni wa kumfata kumpiga picha za kuweka instagram haahahahahhahaha…

Jamani wenzenu mastaa wa majuu wakiwa mastaa hwana haja ya ku kulipa photographer, mapaparazi wenyewe wanakimbizana kila kona kukupiga picha,na kama swala ni quality photos ukiingia online 5 mins utapata picha zako zooote ulizopigwa na media kwa siku hiyo. Wenzenu huku wakitaka kuwa kwenye news  wanawatip off media where they will and what time alafu media wakifika wanajifanya kushtuka sasa na huyu kwa ustaa wake shingongo anatakiwa alipe wafanyakazi wa kwenda hadi zanzibar kumpiga picha Diamond. Ila sasa anamrahisishia kazi maana picha zote zipo instagram anazilipia mwenywe…hahahahahha….KWELI akili ni nywele….

Imagine afanye show, then alipe kila mtu hapo, hivi kweli atafika mbali financially huyu kijana?

Haya maisha anayoishi wanafanya mastaa ambao wana hela mpaka hawawezi tena kuhesabu, yani wameshajenga maisha yao mpaka ya miaka 20 ijayo

sas ahuyu kijana wetu jamani nyumba yake tu bado hajamaliza hizi show off za hivi za nini?

Kila mtu anajua he is big now, he doesnt need to spend money kufatwa fatwa na watu for people to know that…..

Naomba kuuliza hivi ni mara ngapi tunakutana na mastaa wakubwa huku marekani wako public places hawana mabodyguard wala nini????

Nilishamuona Usher mall ila kwa mbaliii  anahang out  na demu wake ukiambiwa ni superstar huamini, hivi kwani hawezi eka bodyguard wa kumfata fata muda wote??

sasa kaka etu hata romantic getaways yeye anafatana na bodyguard na wapiga picha…hahhahahhahaha

Hahhahahahahhahahahhaha……Haki vile….. IMAGINE hapa anawalipia watu wooote hao hotel rooms, na kuwalisha wooooooote ,na ticket za ndege juu hapo bado hajawalipa mishahara… HIVI kijana ana future yoyote huyu kweli? Ningeelewa kama angespend pesa zake kulipa wasanii wakubwa wakubwa kufanya nae collabo kama alivyofanya kwa Davido ila sio kwa picha za kuweka instagram….

Im not a hater jamani, ila sometimes unajua bloggers tukiongea muhusika akasoma hata kama hatopenda ila inamsaidia na atabadilika…

Hivi jamani hii romantic getaway niambie still kabeba wafanyakazi wooote, na wote wakavalishwa white ili picha zipendeze…haahhahahahha

 Nangoja siku nione beyonce na jay Z wako vacation na wafanyakazi wako ,wapiga picha wao ,mabodygurd wame color coordinate nguo zao ili picha zipendeze….

Alafu sasa kapata na mwanamke ambae na yeye ni mpenda mapicha na mashow off so hana hata wa kumshauri maskini…..

Sasa sijui ndo mpiga piha inabidi aamke asubuhi aende chumbani kwa bosi na mke wake wavae ma bathrobe yao awapige picha wanakiss then warushe instagram?hahahahhaha

Duh, kazi kweli kweli….. Kama kuna mtu amewaambia kuwa mastaa wa ulaya ndo wanafanya hivi kamdanganya jamani wenzao wanaviziwa na paparazi tena picha zinakuwa hazina quality sababu ni za mbali mnoooooo. Ukiwa star huna haja ya kufanya yote haya media watauwana kutaka picha zako…

ALafu pia management yake wangemwambia kuwa sometimes wasiwape mashabiki everything they want to see. Keep people curious. HAPo ndo mashabiki wanakuwa na hamu ya kukujua undani wako sasa hawa kila dakika 5 picha soon watu watawachoka kabisaaaa

kama mimi ,mwanzo nilikuwa nawaona hot news kila siku lazma niwaandike ila mpaka habari ikaboa wasomaji wakagoma coz its too much.

Yani anaewadanganya hawa kuwa mastaa wa mbelez ndo wako hivi sijuiii…

Hivi hata hao wanaigeria kina Davido sijui PSquare hivi huwa wanafanya any of this stuff??? Ndo maana wanamuziki wetu huwa hawawezi kumaintain status muda mrefu ni sababu wana loose focus. Yani watanzania alietupa laana yakushow off sijui ni nani… hahahahhaha… Yani tuko tayari kuspend hata last senti kwenye account ili mradi ushow off.

I hope ataichukulia hii vizuri na kubadilisha hili….

Bado ana safari ndefu sana huyu kijana. Hizi pesa anazochezea sababu ya picha za instagram atakuja kuzikumbuka sana later. Hao watu anaowakatia maticket kumfata fata nyuma for no good reason atakuja kuzikumbuka. I know for a fact hakuna mtu anaemlipa kwenda kufanya show akampa na budget ya mpiga picha wake, ya dj wake, ya mameneja wake na ya GF wake. Navyojua kwenye show anapewa budget yake na wacheza show wake.PERIOD……Hao wengine ni yeye inabidi awalipe….

UPDATE….

Mweeeh,haya one of Diamond’s managers amenishushuajeee sasa???????

OMG, Is he for real? jamani si niliwaambia Diamond itakuwa kaambiwa na ma manager wake kuwa kufatwa vile na kundi la watu ndo ataonekana kama big stars wa marekani??? Oneni jibu la manager wake jamani…. Oneno mfano alionipa??? OMG, Yani nimeishiwa nguvu zooooooooote…. Yani nimeishiwa na maneno yooooooooote. Nimeambiwa I know nothing about ent business nikamgoogle LADY GAGA nione alivyo na entourage kubwa ndo niongee…NGACHOKA!!!! Yani nimekosa hata la kumjibu kuhusu lady gaga kama wewe unajibu etu tusaidie pls…

Yani la LADY GAGA limenimaliza sina hata la kuongeza, Hivi huyu manager amelewa au yupo sawa? hivi kweli anajustiy spending ya Diamond kwa kucompare na spending ya artist ambae in 2013 alimake $80 million, pesa ambayo hata kuiandika kwa tsh siwezi maana ntaandika masifuri mpaka nidate, pesa ambayo mpaka Diamond anakufa atakuwa hajawahi kuiona kwenye account yake,, hiyo pesa LADY GAGA kamake in 1 yr jamani na ni pesa ambayo diamond mpaka anakufa hatoishika mkononi alafu ndo mtu kama huyo wanageza swaga zake, si bora wangesema wanamgeza Neyo au Ray Jay mdogo wake Brandi kidogo pesa zao labda Diamond anaweza kujikuna kuna akafananishwa nao. NGACHOKAAAAAAAA……hahahahhahahahah,,

Alafu huyu manager inaonekana anapenda shari alafu sasa ni mwanaume ..Mie sikuongea vibaya nilitoa ushauri hata yeye angeweza kujibu kistaarabu kwa kuweka  hoja za maana sio mambo ya kusema natafuta KIKI or sijui na mie nataka kujoing entourage yao…Kha.. Although wewe unajua kila kitu kuhusu ent business let me tell you kazi ya kubishana na bloggers juu ya Diamond ni kazi ya publicist wake sio kazi yako wewe, so labda ungepunguza mmoja wa mabeba mabegi ya diamond hapo mkamuwekea na publicist kama LADY GAGA….hahahahhahahahhhahahaha…….

Anyways, sina hata cha kuongea maana jibu lako tu limedhihirisha kuwa huna akili hata moja na umesha prove my point kuwa wewe na hao managers wengine ndo mnaomdanganya Diamond. Ila siku ustaa wake ukiisha na pesa zikakauka tunaomba muendelee kumfata fata nyuma hivyo hivyo sio mumkimbie….

Unasema na mie mtanilipa niwe naandika habari za Diamond, sasa kama Diamond kashindwa kukulipa wewe pesa ya maana mpaka mkeo- ESMA amekukimbia kwa  kuchoka maisha ya kubadilisha mboga ndo ataweza kunilipa mimi ??? Mke alikuwa anataka umnunulie Range Rover akakuta mume kumnunulia  Suzuki tu hawezi…hahahhahahahah……Sasa mie mtanilipa nini????hahahahahhaha

Again niliongea vizuri na kusema I hope Diamond ataichukulia vizuri nilisahau kusema I hope manangers pia wataichukulia vizuri.lol… Haikuwa nia yangu kuamsha vagi huko instagram.  Good thing is angalau tumejua ujumbe umefika vizuri kwa wahusika  na hata Diamond akipitia comments za fans wake ataona mawazo yao na nnaamini hata kama atafanya ubishi ila lazma atakuwa anafikiria mara mbili mbili hili na kuna siku ataanza kufikiria ya mbele yasije kumkuta ya Mr. Nice au Saida Karoli, mwanamuziki ambae nyimbo zake  mpaka leo hii zinapigwa ndani ya big movies za hollywood na hana hata shingi mia moja benki nadhani aliuzaga hata rights za huo wimbo wake kwa milioni 2 labda…hahahhahaah…Hii yote inatokana  na mwanamuziki kuzungukwa na mburulaz kama wewe Salaam…….Yani kwa jibu ulilotoa inatosha kuonyesha watanzania in 5-10 YRS time Diamond atakuwa wapi career wise.

Read More
1 2 3 134
Designed by muzemultimedia web design Tanzania