HOLLYWOOD SHOPAHOLICS – ALMOST……

Alhamdulillah leo nimekabidhiwa website yangu na kampuni iliyokuwa ikitutengenezea website na nimeshaanza kupandisha vitu…. It will take me 2-3 days kumaliza na kutoa link ya website ili watu waanze kununua…..

 

Kama unatu follow instagram au kama unasomaga hiyo link yetu ya instagram hapa hapa kwenye blog basi utakuwa unajua tunashughulika na nini….

Basically tutakuwa tunauza nguo,viatu, accessories, etc kwa wanawake na wanaume na baadae tutaweka na watoto….. Tuna vitu vizuri sana na kwa bei ya chini bei ambayo nakuhakikishia hutopata kwingine……

kwa wanawake tunauza wedding Dress nzuri sana kwa dola 500 na kushuka chini, wedding dress zetu nyingi bei ni dola 350-400 tu. Evening dress bei zake ni $150 mpaka 250. Tunauza Maxi Dresses nzuri sana kwa bei nzuri pia,,,,,

Tungependa biashara yetu iwahudumie zaidi watu walioko bara la Africa na walio nje ya marekani ila kama uko marekani bado tutakutumia…

WE SHIP EVERYTHING FOR FREE……. WEDDING DRESSES, EVENING GOWNS AND MALE SUITS WILL BE SHIPPED VIA DHL FOR FREE and will be delivered to your door. All other items will be shipped via standard shipping. More info about this will be on the website under the topic ‘SHIPPING’

Kwa mlio Dar es salaam  tutakuwa na Physical presence there through our partners, vitu vyote vitakavyotumwa via standard shipping vitafatwa pale na kama ungetaka kurudisha nguo au kubadilisha nguo pia unaweza kuipelekea pale. Tafadhali soma policy yetu ya kurudisha na kubadilisha nguo kwenye website.

Nigeria-Abuja pia tutakuwa na Physcial presence through our business partners kwa ajili ya kufanya returns and exchanges……

DAR ES SALAAM

Golden Jubilee Tower – PSPF BUILDING

FIRST FLOOR – NARINDWA’S CHOICE

Ohio Street,

CONTACT NAME: LEAH MGONJA

MOBILE: +255 784 287 757

ABUJA -LAGOS

BELLA’S BEAUTY PARK NO. 5A LINGU CRESCENT

OFF AMINU KANO CRESCENT, OPP NNPC FILLING STATION , WUSE 2 ,ABUJA

CONTACT NAME: ELIZABETH GUPTA

MOBILE: +234  816 660 4893

AS WE CONTINUE TO GROW WE  SHALL HAVE MORE LOCATIONS – INSHALLAH…

Read More

MCHEKI MUME WA DIDA AKIONGELEA KUMTWANGA TALAKA DIDA

Hivi siku hizi ndo imekuwa fashion ndoa zikiharibia mnaenda elezea kwenye media? sijaelewa……

Dida nakuaminia mwakani ndoa ya nne….Chezea Dida wewe…… Mbona wao wanaoa na kuacha kutwa napenda kuona wanawake nao wakivaa suruali….lol…..

 

PS. Wanaume wengine wanachekesha, mtu hela huna alafu unataka kumchunga chunga mkeo,….Hivi mmenotice kuwa matajiri hawanaga hizo za kuchunga mke? maana anajiamini anajua anakulisha anakuvisha  huwezi kwenda popote, wasio na pesa sasa? uwiiii ni headache atataka akugande ka luba maana anajua dizaini akitokea mwenye nazo waweza sepa…..lol……

 

UPDATE…….

 

Haya mlioshindwa kusikia jana hii ya leo iko poa. Bongo ni noma mwanaume anasema kabisa kwenye video nilimchampa vibao na nikamchapa na mikanda kwenye makalio and nobody does nothing….. Kukaa ukae kwangu mikanda unitandike, hapana aisee….

Nimeona kuna wale wanaosema huyu kaka anaonekana mtu fresh kutokana na maelezo yake kwenye video ila Dida ndo hana heshima, naona nyie hamuwajui wanaume. Hata siku moja usim judge mwanaume akiwa kapupu, mjudge mwanaume akiwa na pesa. Wakiwa hawana kitu wana jua maadili yote, Quraan nzima wanaijua, dini wanaiheshimu, wake wanawaheshimu yani wewe mwanamke ndo utaonekana chizi, sasa subiri apate pesa ndo utamjua yeye ni nani hiyo dini ataiwekea na remix zake mwenyewe na hivi mwuislamu basi akuletee na bi mdogo…… Embu ulizeni wanawake waliotoka mbali na waume zao walioanza nao tangu wanapanda mabasi wengine wanakwambia mume wake alikuwa kashika dini hata pombe hanywi baada ya kuzipata weeeeeeeh ni balaa. Kwa hiyo hata huyu mume wa Dida lazma awe mpole hivyo na mkarimu na kutaja mambo ya Quran sijui nini, ikitokea siku akapata pesa ndo true colors zake zitatokea……. Lazma awe na busara hivyo mtu unaishi kwa mwanamke alafu ujitie mjanja si ndo maana inabidi awe mpole…..

Ila na huyu kaka nae iwe fundisho kwake  next time aende akachukue mke kijijiniiiiii amlete mjini, yani mwanamke atamweshimu vile anavyotaka yeye, maana akifikiria mume wake kamtoa kijijini kamleta Daslam, kamnunulia weaving hata zile za wachina za sh. elfu 8, uwiii mwanamke mbona atamwamkia na yeye kweli hapo atakuwa baba mwenye nyumba na heshima zote anazotaka atapewa ila akienda tena kuoa mwanamke aliemzidi akaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke alafu afikirie atakuwa anatengewa chakula mezani na kuwekewa maji bafuni akaoge atakuwa hayuko serious….. Amake sure next time yeye ndo provider la sivyo itakuwa kila mwaka anaenda magazetini kulia lia mke hamweshimu……..

Read More

HII IMENIUMA………

Mtu kanirushia hii whatsapp sasa hivi nikasema ngoja niwapostie fasta then niendelee na mambo yangu….

Aiseee imeniuma sana, Pole Ray C… I love TID ila hapa kaboa kwa kweli… Duh……

Hivi kwani kuna historia hapa mbona sijaelewa?

Read More

DADDY’S PRE-BIRTHDAY LUNCH @ THE IVY BEVERLY HILLS…….

Kwanza kabisa naomba nianze kwa kujieleza kwa nini nimepotea kabisa humu hata comment sijacheki…..

Wapenzi niko busy kupita maelezo, kuna project im about to launch, kwa kweli inanidatisha……

Naingia kulala saa kumi usiku na kuamka saa mbili asubuhi for almost 2 weeks now… Yani nimechoka vibaya mno ndo maana leo

nimeshindwa hata kuvua sunglasses maana uso umechoka makeup zinadunda, nimeamini kulala ni kitu cha msingi sana kwa binadamu.

Please pray for me hii project itake off, kwa kweli itakuwa ni project ya aina yake…….

Kuna wanaoniambia kuwa ku update blog si kitu cha dakika moja tu, aisee hamjui huwezi kublog kama hujui current affairs za bongo na za dunia nzima which means lazma nitumie muda kukaa online, kusoma news, other blogs, instagram, etc all that takes time whichi dont have right now..

Nipeni muda ntarudi full force humu mpaka mtafurahi na roho zenu…..

Waislamu wenzangu nawatakia Ramadhani njema, mwaka pia sitofunga kama mwaka jana, mwaka jana nilikuwa mjamzito, mwaka huu nanyonyesha,

yes na madiet yote nayofanya bado nayonyesha exclusively, nilijaribu ku suppliment na formula ya enfamil sababu ya mitikasi yangu ila dogo amekataa kabisa formula, yani ukimpa analia kama kafinywa, hata awe na njaa gani hanyi,so bado nagawa nyonyo full time, basi na hizi diet zangu sometimes nasikia kuzimia.

Nimeanza kunywa pre-natal vitamins zangu upya sababu nimeambiwa kwa vile sili vizuri zile zinasaidia kuweka vitamins mwilini….

Uwiii kweli diet imeanza fanya kazi cheki kishingo kilivyoanza kuwa kirefu tena….lol

Kesho ndo birthday ya my mume ,tumesherehekea leo sababu kesho ni working day…..

Tulimpeleka sehemu moja very upscale, very trendy in Beverly Hills inaitwa THE IVY,

Wanna know how upscale it is? There is a Chanel store right next to it….lol….

Its so funny how people were lunching with Chanel shopping bags pembeni ya meza zao…lol…

This floral print Maxi dress will be available soon for sale…….

OMG I love love love this dress? Yani leo wanawake walikuwa wananiuliza nimelinunua wapi kwa kweli

kila mtu alilipenda……… (I hope sijaiba slogan hapo)…lol..

Mama Watatu, gauni kubwa sio size yangu ,size yangu kwenye maziwa haifungi…hahahha

mwili mdogo ziwa la mtu wa size 14…hahahahhaha

OMG how beautiful is this dress..Nimedata nalo…

We will have it in S,M,L XL

This time vitu vimeenda shule….lol..

Na bei zangu zimezidi kushuka….mtafurahi mwenyewe

Wanangu mie….. Keanu and Bhoke…..

Jamani mtoto anabusiwa huyu nahisi anatamani kutuambia tuache anashindwa..lol

A

Awwwww

My 3 beautiful kids…. Im blessed…..

Mwanangu Kenzo, viatu vya Kenzo soon vitakuwa available for sale…..

My swagalicious son, basi watu wanalivyokuwa wanamsifia kapendeza,mpaka mawaiter walikuwa wanamsifia

basi mwanangu bichwaaaa…hahahaha

My life……

Bday boy and his last born….

Mama na wana….Uwiii nawapenda wanangu….

M

Kenzo alinunaje sababu tulisimama for a long time kusubiria table,

ndo mambo ya The Ivy hayo wana wateja wengi kiasi kwamba unafanya booking na ukifika waweza simama for 30 mins ukisubiria meza….

Kenzo’s loafers will be available for sale soon…. I will have load and loads of cute loafer for children wa kuanzia 2yrs mpaka 10….

My chubby baby, uwillll jamani toto langu lipo kama doli…hahahahhahah

yani namkisigi vimiguu vyake mpaka basi.

Awwwww, Keanu baby… Jamani toto langu zuri acha tu niseme….. hahahahhahahaha

kako so cute na uchubby wake ila tatizo kumbeba sasa, uwiiii dakika 5 tu mikono inauma…hahahha

Besties…

Lunching at The Ivy with my family……

Duh nawapenda hawa watu jamani….lol..

First born and last born…Mwaaaah…

Keanu baby….

Keanu shavu dodo…lol..

Happy birthday to you….

Cake by Hansen Cakes – Beverly Hills…..

Kenzo leo ujanja wa kupuliza mishumaa ya cake za watu ulimuisha maana alikuwa anasema “moto moto”…

Hahaha nimemtoa ushamba bora next time hato sema moto….lol..

Daddy’s cake is by Hansen Cakes- Beverly Hills,

Watu wangu…

In love with kENZO’S HAIR…

Jamani wamarekani wanaboaje eti hawakatagi cake wala kulishana, yani mkiimba tu eti waiter anaifata cake

anaenda jikoni kuikata kata mwenywe anawaletea kwenye visahani, wabongo mpaka ukate cake ulishe watu, bday ya Bhoke

we niliwaambia no way lete kisu hapa akate cake atulishe sie waafrica..hahahha Hubby leo amekataa kata kata eti “Americans dont care about cutting

cakes we only care about taking over the world” …hahahahhahaha nilicheka, mume wangu chizi…

Haongei tena…lol

h

Hahaha Model Kenzo akinipa mapozi… Chinchila ndani ya picha kama kawa…

Mama na mwana…

Alhamdullilah, I love my family…….

Read More

CORSETS ZIMEFIKA

Hey wapenzi wangu,

Mzigo wa corset ushaingia nautuma  kesho

Ntaweka post ingine ya maelezo mkachukulie wapi etc…..

kama kawa kila corset itakuwa na jina ,ukifika unawapa jina lako wanakupa….mwaaaah

Read More
1 2 3 101
Designed by muzemultimedia web design company los angeles