SO SWEET!!!!

Hapa tulikuwa Warsaw, Poland kwenye kambi ya Miss World 2006.  Yeye alitangulia Poland, mimi , dada yake Sunna Sepetu pamoja na kamati ya Miss TZ tulienda Poland a week before miss World.

Hapa nilikuwa nimeenda kumuona kambini , nilipewa just 1hr kuongea nae na kupiga picha then arudi kwa wenzie….

Aisee hii b’day message imeandikwaje kwa hisia nzito…. Yani imetoka moyoni…..

THANK YOU FOR THIS TOUCHING MESSAGE DOGO AKE…….

You are just the realest thing out there. 

I HAVE BEEN YOUR NUMBER ONE FAN FROM DAY ONE….

Goddamit I f***ing love you moreeeee……hahahahhahahaha

Read More

MY 35TH BIRTHDAY……..

Birthday girl….

Mama watatu…

Me and my mdoli…hahahaha…

Mie na kitinda mimba wangu….

Awwww,happy baby….lol..

Uwiii watoto wote hawa nimewazaa eti???? uwiiiii uzeee.com.lol..

Bhoke alituharibia picha na macho ya kulala tukamkatilia mbali…hahahhaha…

Basi leo ilikuwa balaaaa,mnuno wa Kenzo….

Eti kwanini Keanu kavalishwa bow tie na huku yeye hajavalishwa?

Akaniambia mie “mommy you don’t love me, you love Keanu. That;s why you didnt get me a bow”

anaiita bow wala sio bow tie… Jamani sikujua hata kama bow tie ingekuwa issue kwake maana keshazivaa mpaka basi…

duh,nimekoma leo…

hapo ni tunadaiwa ‘BOW” ndo kieleweke… Hacheki na kima….lol

Mwenzie kanuna yeye anachekelea na “BOW” yake….

Huyu ndo dogo alietuharibia siku……

Awwww, my people….

Kenzo hacheki na mtuuuuuu… Full mnuno….

Jamani katuharibia picha leo Kenzo….Eti akasema tumvue Keanu tumvalishe yeye….duh!!!

Sasa mwenzie hiyo “bow” imekuja na hiyo outfit yake tunamvuaje kwa mfano? alafu yeye isingemtosha…Mweeeh..

Kaka mtu amevurugwaaaaaaaa…hahahahhaha

Ngoja tupige picha na asie nuna sie…

Uwiii Keanu lakini kama kazidi ucute sasa…hahahhaha…

Kama kadoli vile…

Sie na mwanetu ambae hakutununia…Tulichoka haribiwa picha na mtu kanuna tuuuu….

Baba na kijana wake asienuna….hahahhaa

Hey Keanu…

Too cute these 2…

Awwwww….

Hahhaah, leo tumecheka so we went to Calfield’s in Beverly Hills for dinner,

sasa tukakuta watu kama 10  tu humo ndani maana leo Wednesday…..Ila tuliinjoy kupiga mapicha bila kumkera mtu…lol…

Dadi ake amesharudi L.A ila now yupo busy balaaaaa hata ukimbeep hakupigiii…..

Anafanya mitihani ya GMAT coz anaanza soma a dual masters degree ya MBA & Real Estate kwa pamoja…..Yani hawezi kumake partner kwenye kampuni yoyote ile bila Masters so imebidi arudi shule na kaamua kusoma MBA sababu ataka apate executive position popote pale…

So the next 2 years will be the hardest for us…. Maana daddy atakuwa shule full time at the University of South California….Uwii ila akimaliza hiyo program atakuwa hot hot hot hot cake ukiweka experience yake na hizo masters mbili,uwiii itakuwa noma…..Tumuombee sasa amalize salama,,,,

Awww, toto and daddy….

REAL MEN WEAR PINK……

Hiki nako kitakuja sukumwa hukooooo….Mtu kanuna sababu yake alafu anaenda kumuegemea….

Awwww, busu from  super sister Bhoke….lol..

Aww, too cute these 2…

Wanangu…

The last 10 days nimepungua sana…..

Jamani mazoezi siyawezi mie mvivu sana so najishindisha njaa mpaka nakoma….lol..

Hahahaha, muone anacheka na pengo lake….MWEEE mtoto alitukosesha raha huyu leo mpaka ikabidi tumbribe tu akaacha…

Kesho nampeleka target akanunue toys…. Yani kuambiwa hivyo ndo kikaanza kucheka…MFYUUU..

Sasa hiyo kesho ntakavyosumbuluwa jamani ili twende huko….DAH…

Toto….

US…

MY FAMILY…. BILA HAWA HAKUNA MIMI…….

MAISHA NDO HAYA…..

Muonze mzee wa ku blow candle za watu alivyo ready….hahahahahhaha

Legs for days!!!!

The princess of our home….

Mommy’s princess……Wenye kumbukumbu sijui mtaikumbuka hii nguo…

I wore it once only tena  5yrs ago in Dubai kwenye white party ya kwenye boat on Tania’s birthday…..

Yani toka niivae kwenye ile birthday niliitupia wapi sijui…Leo nashangaa mtu kaibuka nayo…hahahahhahaha….

Anyways siwezi tena kuvaa kinguo cha kibaby hivi bora kakichukua maana kingepotea au ningekigawa tu…..

Yani anadataga na nguo zangu anasema she cant wait to turn 16 avae my heels na nguo zangu…hahahahhaha

Leo tulimwacha avae heels zangu sababu alikosa flats za kumatch na hiyo nguo….Alifurahije sasa maaana anajua haruhusiwi kuvaa heels na nguo flani flani..Kadata leo nahisi ataota maana hazioni tenaaa hizo heels….lol….

Toto ake mommy…..

Me and my young lady…. Jamani mwanangu ananipita urefu kama hivyo….

America’s next top model….love her to bits…

#LEGSFORDAYS

So After dinner, daddy decided he wants to go to the Beverly Hills hotel for a few beers…..

Tukaenda, uwiii Beverly Hills hotel wanajifanya, tulinyimwa kupiga picha humo maana kuna so many celebs hapo na wealthy people

so no pics tena ule mcamera wangu ndo kabisaaaaa…lol…So tukajitokea zetu nje tukapiga picha……

Hahahah these 2 wanapendanaje sasa….lol..too cute…

US….

Jmaani Keanu anaboaje sasa, Mtu kaanza kusimama like 2 months ago and 3 weeks ago kaanza kutembea. Anatembea 3 steps anadondoka ila leo

eti leo kagoma kusimama mwenyewe nimpige picha na hizo nguo zake…Kaniuzi.Ukimsimamisha tu huyo anatambaaaa….lol….Nikamwambia simnunulii tena pamba nzuri mpaka atembee mwenyewe ,EBO!!!!

Ok simama Keanu, simama ..pleeeeaseeee….

Muone anavyojidondosha jamani…hahahahah..

Yani nimechukua…lol…

Daddy and his boys…

Kila mtu anaekwenda Beverly Hills hotel lazma apige picha hapa ….

MY BABY……

Mama mtu full kufunikwa

BABA NA MAMA WATATU….

GOODNIGHT…..

Read More

BANANGE ! WAGANDA WANAMSHOBOKEAJE JACK PEMBA……LOL

Jack Pemba kwa sasa anaishi Uganda… Sijui ndo zile long vacation zake za kama mwaka hivi then anarudi UK, sijui…lol..

Ila ndo hivyo gosspit media za Uganda habari ni jack Pemba, wanamwita “new money bag in town”

hahahahahhahaha…. Wangewauliza wabongo kwanza habari za Jack Pemba….lol…

Unaambiwa juzi kati kafanya bonge la besdei party lenye theme ya OO7 ,wanasema katumia 100m ya Uganda…hahahhaa

kabla ya besdei unaambiwa  alitumia Johnie Walker kuosha gari yake….hahahahahhaa…Waganda wamedataje nae sasa…..

Ila kweli wanawake taste zetu zinatofautiana, hivi kweli unaweza kutoka na mwanaume anatumia kinywaji kuosha gari lake? doesnt matter ana utajiri gani but kwa kufanya hivyo tu inakwambia akili zake zipoje…..hahahaha..Pia inakwambia hana hela za kivileeeeee, matajiri wanauchungu na pesa zao wewe, matajiri ni wabahili. Hawachezei pesa. 

Ila mie nampendaga sana Jack PEMBA wakati naandaa mambo ya Miss TZ nilikulaga sana mihela yake…hahahahahahahaha……

Yani alikuwaga mshkaji wangu balaaaa…. Ilimradi nimstue aje kwenye mazoezi aangalie mademu amwage mahela hapo basi…Alafu enzi za chuo laki 5 mtu unaona kama 5m…hahahhahhahahhaha,,,,,,, Yani alikuwa mshkaji wangu mnooooooooo.

Cake yake ndo hiyo ilikuwa na theme ya James Bond 007…hahahahaha..

Na mwenyewe mmeona nguo zake match na keki….hahahahaha

Unaambiwa ndo aliingia hivi ukumbini na boti …hahahahhahahaha…huku akiwapungia wageni..

Jamani Jack Pemba anashughuli….lol

Dadake huyu wanasema alitoka Tanzania kwenda msuprise kakake huko Uganda…

mmeona bango la 007???lol

Unaambiwa Jacky kajiopolea Ugandan singer , Desire yule wa BBA….

Jacky anapenda mastaaa jamani…Yani wanawake wasiojulikana yeye hawataki…

Huyu Desire nae angemuuliza Aunty Ezekiel habari za JACK PEMBA… Atazalishwa hapo na kuolewa harusi kabisa ila siku ya kurudi UK ikifika atasoma number….hahahhahahahahhahahaha…. Chezea Jack Pemba wewe….

Hivi kwanini kaikimbia Tanzania kaamua kwenda Uganda kutumbua??? mnaojua why  tujuzeni please… Maana hii sio haki jamani, nchini kwake mbona kuna mademu kibao tu who need a guy wa kurusha mahela kama  yeye alafu anaenda wapa waganda?hahahahhahaha

Read More

RAY BAN MIRROR GLASSES GIVEAWAY……..

Uwiii jamani sijawahi nunua sunglasses zikanichukiza kama hizi… Yani hazinipendezi hata kidogo….

Nikasema nimpe Bhoke, akasema eti haipendi…hahahahhahaha..Mtoto mshamba yani eti hapendi…lol..

Na Bhoke akikwambia hapendi kitu bora ukichukue maana atakicha popote Kenzo na Keanu wakichezeee…..

So nikaamua kuwagawia mawaziri wangu…..

Yes mawaziri, kaeni mkao wa kula… Nayatuma bongo kesho. Next week yatakuwa mujini then tutafanya kama tulivyofanya nywele…….

So March 15th ndo itakuwa siku ambayo ntawatangazi miwani iko wapi then ukimbie ukaiwahi…

Niliinunua Nov last yr wakati naenda bongo . Nimeivaa  less than 5 times maana kila nikiivaa nakuwa sijisomi…

I bought them for about $200…

Perfect skin…….. Nimeacha mambo ya creams,sio za kung’arisha wala za kuwakisha……lol..No obagi wala nini…

Natumia moisturizers only and a good face oil…. Makes my skin soft and have a natural glow…..

Kenzo anawapa hie jamani…lol…

Mawaziri only ndo wanaweza kushiriki……

Inabidi unitumie email unipe jina lako la uwaziri ili nikupe password….. Ukiona sikujibu email yako ujue uwaziri wako wa utata….Yani kuna wenye ID ila wanazitumia once a month. Hao sio mawaziri..Naongelea die hard mawaziri……..

email: mangekimambi@hotmail.com

Read More

MAONI YANGU JUU YA ALI KIBA’S NEW SONG – CHEKETUA…….

mmm

Aisee ngumuje kupata time ya kufanya biashara, kulea familia then kublogua???? Nakomajeee…

 Anyways,  leo nimepata chance  ya kusikiliza nyimbo mpya ya Ali Kiba fasta fasta….

I like Ali Kiba’s music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za zamani… Au labda tuseme yani  nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina tofauti.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo sana…… Nyimbo zake za zamani zilikuwaga nzuri sana , ila pia yawezekana za sasa hivi zinaoneka sio nzuri sababu zimefanana na za zamani…Yani nyimbo ya Ali Kiba hata uamshwe usingizini bila kusikia hata sauti ukisikia biti tu unajua nyimbo ya Ali Kiba….lol….

Kwenye issue ya kiwango cha nyimbo kushuka hayuko peke yake hata besti ake  Diamond pia nyimbo zake zimeanza kushuka kiwango…. Mie naona tatizo lipo hapa…. Ni kwamba wamesha maliza material zao zooooote  nzuri…. Ni sawa  na kwenye mashindano ya kukimbia unapoanza kukimbia unakimbiaje fastaaaaa kama gari vile, ila mwisho wa mashindano nguvu zinaisha unaweza hata anza tembea…Mie naona ndo kama hawa vijana, wameshaandika all the best stuff they have sasa material zimekwisha inabidi wafanye tu ili mradi watoe new single….

Yani kwa Ali Kiba kwa jinsi alivyo under pressure sababu ya hiyo ya likinganishwa na Diamond naona hii new single imemwangusha kabisa yani na sasa ni dhahiri kuwa yeye ni number 2. 

Well, kunapokuwa na tatizo lazma tutafute na suluhisho… Tumeshajua tatizo sasa hivi ni unandishi wa nyimbo sio kwamba hawajui kuimba kama zamani. Talent zao zipo pale pale au hata labda zimeongezeka kutokana na experience ila problem is hawana tena material ya kuandika nyimbo. I think hata VANESSA MDEE  na  JUMA JUX   wanaface   the same problem. Yani Vanessa na Juma Jux wana swaga za hatariiiiiiiii, yani wamekaa kimamtoni ile mbayaa ila tatizo ni nyimboooooooo, nyimbo hazina viwango vileeeee…..Well wafanyaje sasa???

I think hapa mie nimeona kuna fursa kubwa sana ya uandishi wa nyimbo Yes asilimia kubwa ya artists wengi wa marekani huwa wanaandikiwa nyimbo zao. Especially baada ya kuwa kwenye gemu for a while maana na wao huwa wana run out of material au aideas ndo hapo inabidi wanunue..

Kwa mfano one of the most popular hits in the world ule wa I will always Love you wa Whitney Houston – yeye aliununua tu,ule wimbo uliandikwa na mtu mwingine. I think uliandikwa na Dolly Parton. So kama Whitney angetaka sifa za kujifanya yeye anajua kuimba na kuandika songs zake mwenywe basi sidhani kama angejulikana dunia nzima kama alivyojulikana baada ya huo wimbo alioununua kwa Dolly Parton.  Au tuseme Michael Jackson, mnaikumbuka ile nyimbo yake ya Thriller wakati tuko watoto tulikuwa tunaipenda balaaaa, na ilikuwa number 1 hit all over the world. Guess what Michael Jackson hakuandika ule wimbo aliununua kwa mtu anaitwa Rod Temberton.

Yani kuna watu wanakuwa mamilionea kwa kuandikia waimbaji nyimbo. So jamani mie naona its time sasa watokeee professional song writters Tanzania waanze kuwaandikia hawa waimbaji wetu nyimbo. Kama sio hivyo ndo hivyo wataendelea kutoa nyimbo zisizo na viwango mpaka mwisho watasahauliwa maana kuna new artisits ambao wana nyimbo zao mbili tatu kaliiiiii watatoa tutawapenda then tutawasahau hawa.Kama wanataka kubaki on top of the game for many years inabidi waanze kununua nyimbo sasa.

Although kuwa song writter sio lazma wewe mwenywe ujue kuimba ila hawa waandishi wa nyimbo wengi wao na wao pia wanajua kuimba ila for some reason walishindwa kutoka so wakaamua watoke kwa njia ya kuandika nyimbo…. Yes, its unfair ila sometimes kuna nyimbo ukiimba wewe usiejulikana itaonekana mbaya ila akiimba Ali Kiba itakuwa number 1. so instead of kukosa vyote kama hujatoka wewe kama star kwanini usitoke kwa njia ya kuandika nyimbo ? kama ndo talent yako? Na wewe utakuwa star kama huyo anaeimba nyimba zako maana lazma aseme kuwa nyimbo ni ya kwako au kama vipi mlipane pesa ndefu sanaaaaa ili afiche kuwa kaandikiwa nyimbo which mie naona ni ujinga sababu kuandikiwa nyimbo sio kitu kibaya at all it only means you only want the very best hutaki kutoa nyimbo sizizo na viwango.

So wenye vipaji vya kuandika miziki anzeni kuandika muwape hawa watu maana yani wana full vipaji na video zao zimeenda shule ila sasa nyimbo zao zinawa let down ile mbaya…..

Kwa mfano VANESSA MDEE, natamani mtu amwandikie songi moja kali la R &B in english, uwiiiiii mbona atakuwa African sensation au hata world wide sensation over night.  Maana swaga zoooooote za kimamtoni anazo….

John Legend pia ni mwandishi kabla hajatoka alikuwaga anawaandikia mastaa nyimbo mpaka siku moja alipiamua asiuze nyimbo yake aimbe yeye mwenyewe ndo akatoka kama mwimbaji. 

Alafu kama mmenotice wasanii wa bongo hawatoi albums at all. Wanatoa single tuuuuu… Kama huyu ali kiba alivyofanya come back si alitakiwa atoke na bonge la album,instead akaja na single mbili. That again shows kuwa hakuwa na enough material kutengeneza 14 songs za kujaza album. Which shows kuwa waandishi wa nyimbo wanahitajika sana. Aisee its important for ana artist kutoa album jamani sio career yoote anatoa single tu. Our top artist Diamond ana album moja tu, how sad is that? Inasaidia hata show zako kunoga coz unakuwa na nyimbo mpya kibaaaa za kuimba. La sivyo kwenye show unaimba nyimbo mbili mpyaa zingine zooote za mwaka 2000. Again ntatoa mfano wa diamond, sijui kama wangapi wana CD ya ile album yake ya kwanza, uwiiiiiiii, jamani that album is crazy goood. Asikwambie mtu,jamani album ina nyimbo nzuriiii ile.  Uwii kuna nyimbo moja inaitwa kizaizai kwenye ile album uwiii naupendaje sasa???? So now Diamond akifanya show he has 2 new songs and the rest inabidi aimbe nyimbo za 4-5yrs ago sababu hajatoa album in a long time… Againa tunarudi pale pale sidhani kama ni kwamba hapendi kutoa album ila tatizo ni kupata nyimbo 14-18 za maana za kujaza album… So again, waandishi jitokezeni I think kazi zipo sanaa tu… HATA Ali Kiba nae ni same problem akifanya concert ni anaimba 3 new songs ambazo ni mbaya then the whole other time anaimba nyimbo zake zilizohit more than 5 yrs ago.Jamani nilienda conrcet ya Rihanna 2 yrs ago.. Uwiii,unajua mdada for 1 hour anaimba 1 new song after 1 new song, tena ndo nyimbo zinazihit at that time, mnakuwa mnazijua word by word, yani hapo kwenye concert nyimbo zoooote alizoimba ni zinahit all over the country hiyo ndo inaitwa tour. Sasa wabongo anasema anafanya tour huku ana 2 new songs nyimbo zingine zoooote za mwaka 47. Toeni albums jamani, lipeni watu waandikieni

Kwa kifupi na chosema ni kwamba kuna need kubwa ya song writters Tanzania. Na pia wasanii wetu ambao wameshajenga majina yao wasikubali kushuka kwa kung’ang’ana kuandika nyimbo zao wenyewe. Waaenze kutumia professional writters ili waendelee kubaki kwenye gemu…..

I swear nyimbo za Ali Kiba nimezichokaaaaaaaaaaaaa, nimezikinaiiiiiiiiii. YANI ZIPO VILE VILE ZOTEEEEEE…. Na Diamond nae asipoanza kununua nyimbo au kuandika very good songs  nyimbo zake zitaanza kuboa kama za Ali Kiba soon washangae vitoto vinakuja juu vinawafunika kwa kutoa great songs.

Read More

ETI MADAM KAENDA FANYA NINI SINGIDA????

Eti kidole cha ndoa cha madam kina nini vile????

Huko Singida madam na family yake wanasherehekea kitu gani ati????

Mie mwenyewe sijui ndo maana nauliza…..

Read More
1 2 3 134
Designed by muzemultimedia web design Tanzania