NANCY SUMARI- TAFADHALI ELEWANA NA DADA YAKO……..

Yani imenichukua muda mrefu sana kuweka hii posti mostly sababu both Nakaaya and Nancy are my dear friends….

Ila sio ule urafiki wa ukaribu kiasi kwamba naweza kuongea nao in private kuhusu matatizo yao binafsi au naweza kuwapatanisha. Siko nao kihivyo..

Na kwa kweli nashindwa kuelewa why rafiki zao wa karibu wanashindwa kuwapatanisha…… DAH….

Kwanini nimeweka hiyo heading first of all , I know for a fact NAKAAYA anampenda mdogo wake kufaaaaaaaaa, uwiii anaweza kufa juu ya Nancy, Pili mimi ni first born kwa baba yangu najua navyowapenda wadogo zangu na nikikwaruzana nao kidogo tu huwa naweweseka mnooo yani silali ,sili mawazo tu ndo maana nikasema NANCY aache kumtesa dadake, Tatu I know for a fact chanzo cha mwanzo kabisa cha ugomvi wao ni Nancy ndo alimkosea dadake vibaya mnooooooo, yani kwa kile Nancy alichokifanya dada yake ndo alitakiwa awe ana act Nancy anavyo act right now. Siwezi ongelea Nancy alifanya nini maana siko hapa kumchafua Nancy au kumwanika.So tusonge mbele…….

Nne najua for fact how much Nakaaya amejarubu kuwa karibu na Nancy ila inashindikana, tano hawa wawili nimewajua when they were both nobodys hapo mjini…

Siku ya kwanza nimekutana na Nancy na kumuomba aje kushiriki Miss Tanzania alikuwa na dadake Nakaaya tena siku hizo tulikuwaga tunamuita GLORIA, hilo la Nakaaya naona lilikuwa alipoingia kwenye mziki. Yani Nancy alikuwa hawezi fanya kitu bila dadake, na dadake alikuwa protective na mdogo wake mpaka basi. Ndo maana roho inaniuma nikiwaona hivi maana najua how close they used to be. Jamani hawa watu walikuwa close kupita kumbi kumbi. 

Nancy alinipa condition za yeye kushiriki miss Tz, alikuwa yupo Dar kutembea tu na walikuwa wanarudi kwao in a few days akaniambia kama hana pa kukaa Dar nkamwambia poa ntatafutia pa kukakaa Dar, akasema lazma na dadangu lakini.Imgine walikuwa that close yani Nancy hawezi kuishi hata one day mbali na dadake. Yani toka hana jina wala hakuna anaemjua mjini dadake ndo alikuwa her # 1 fan. 

Ugomvi ni wa long time kweli toka kipindi kile Nakaaya katoa ile single ya kwanza, wakaja kupatana I think mwaka jana naona tena sasa hivi chaliiiii…Nilikuwa napotezea macomment humu ya watu wanauliza vipi hawa wadada. Jana kuna watu wametuma tena comment wanauliza whats happening btwn Nancy and Nakaaya na nilizirusha na nikasema leo ngoja niongeleee….. And the reason naongelea hapa kwa blog ni sababu najua now that issue iko nje basi Nancy will make an effort kuelewana na dadake na dada mtu vile vile ataweka nguvu kuwa na ndugu yae… Eeeh mastaa wa bongo mie nawajua hawapendi kabisa negative things zao ziwe nje  yani ikiwa hivyo they will do everything to change. Nakumbuka 2 yrs ago wadau walikuwa wanatuma macomment humu kuhusu Flavianna kumchukia Millen,uwii mbona sasa hivi wameelewana na wanasupportiana so naamini hii posti pia italeta matokeao mazuri sana……So hata kama Nancy akinimind najua baadae hasira zikimuisha atarudi kuwa mdogo wangu kama zamani coz I really love her…

Alaafu walishapatana maskini sijui hata imekuwaje tena, ila hata walivyopatana last time ilikuwa ni Nakaaya ndo anastruggle kuwa close na Nancy, mdogo mtu hana habareeeee. Maybe sababu yeye maisha yamemnyookea zaidi ya dadake sijui…… Ila Nancy najua unasoma hapa, sikuhukumu  kwamba wewe ndo mkosaji ila najua kabisa Nakaaya anataka kuwa close na wewe ila wewe ndo hutaki….It doesnt matter una sababu gani za kutokuwa close na ndugu yako, yani it doesnt mater nini kilichotokea, ila lazima uyamalize matatizo na ndugu yako. Ni aibu kubwa, watu wanawachora ,wanawasema pembeni bora mimi nnaewaambia. Mnachekesha huko instagram, bora kama mngekuwa hamko kwenye masocial network watu wasinge notice ila iko wazi. birthday ya mwanao Zuri, dadako kimya  ila 2 days later akampost mtu mwingine happy birthday,hizo tuzo zzowatu dadako kimya  anafanya yake na wewe unafanya yako.Rafiki zako wanaposti kwenye insta zao kusupport event yako ,dadakoa naposti mambo mengineee kama hamjuani vile…

Nancy, let me tell you this, the only real,true friend you have ni ndugu yako…..hata ukifa leo hii NANCY, shoga zako watakuja msibani na sunglasses na watalia machozi matatu each, guess nani atakuwa anagalagala chini kwa uchungu??????NAKAAYA!!!! Because ni damu yako, after 10 yrs guess nani atakuwa anaenda kaburini kwako kusafisha??? NAKAAYA, hao shoga zako watakuwa washasahau hata walikuwaga na rafiki anaitwa Nancy. Wewe na Luca mkifa sasa hivi guess nani atamlea ZURI,NAKAAYA. Hakuna rafiki yako hata mmoja atakaemu adopt Zuri, ila NAKAAYA Zuri ni mwanae atamsomesha, atamlea….Ndo maana nakwambia unamnyali mtu ambae anakupenda kuliko wooooote….. You might have fancy friends but undugu ni kitu ambacho huwezi kuweka thamani ndani yake…. Na wewe ni mtu mwenye experience na marafiki, si ulikuwaga very close na kina Irene Kiwia mbona mliishia mahakamani na mpaka leo hata salam hampeani? so ujifunze, urafiki unaweza kuisha anytime, ila undugu ni forever, mtagombana, mtadundana ila mwisho wa siku damu yenu ni moja…Hiyo ndo tofauti ya ndugu na rafiki. Sisemi rafiki zako sio real friends,hapana. Im sure they are.Ila mapenzi yao kwako hayawezi kufika hata nusu ya mapenzi aliyonayo Nakayaa kwako.

Usimdharau dadako sababu labda hayuko fancy kama rafiki zako, naamini Nakaaya angekuwa kaolewa na Manji sasa hivi hata Luca angewakalisha chini akawapanisha ila now mnaona what for. DON’T DO THAT….. 

Huwa nacheka sana watu wakiandika humu eti Mange hamtaji mamake sababu maskini? kha!!! Mamangu kafariki 3 months after meeting my husband,Nilimtoa LANCE  Dubai nikampeleka Dar kumuona mama yangu maana mama yangu alitaka kumuona huyo mkwe aliemtumia zawadi ya swichi , hahahaha gosh,siku tumempa hiyo zawadi alikuwa anasema ,” jamani na mimi nimepata swichi yangu” hahahha. She died. just 6 months after kupewa swichi yake…..R.I.P MOM.

Mtu asieweza kumpenda ndugu yake wa damu hawezi kumpenda anyone else in this world. Sio kwamba Nancy hampendi Nakaaya ila anaweza kuwa karibu na dadake akitaka….Msiseme nimebase sana upande wa Nakaaya jamani najua Nakaaya anavyompenda Nancyyyyyyy ndo maana naongea hivi.Najua anavyoumia kuishi hivi na Nancy. Na watu wa karibu na Nakaaya wanasema baba watoto wa Nancy ndo anachangia sana,yani yeye anataka Nancy awe close na watu wenye uwezo tu so hata Nancy kutokuwa na dadake yeye ana support ……… Sijasema ni ukweli, labda ni maneno ya watu, ila mie naona Luca anaweza kumfanya NANCY akawa karibu na dadake siku yoyote ilee. Especially coz chanzo cha mwanzo kabisaaaa cha ugomvi mwenye makosa ni NANCY. 

Hivi wazazi wao wanatesekaje jamani kuona mabinti zao wanaishi hivi??? DAH…..

Nancy  kama rafiki zako wanakupenda pia wangekushangaa kutokuwa na dadako na wangekushauri uelewane nae, hivi huoni Faraja jinsi alivyo close na dadake although ana marafiki? au KLYN jinsi alivyo close na ndugu zake kwanini wewe ushindwe?? Watu wanalilia kuwa na madada na hawana au wengine dada zao wameshafariki wanawalilia dada zao mpaka leo, wewe unae dadako wa baba mmoja na mama mmoja na humtakii huoni kama ni kitu kibaya sana ?

Hakuna kama ndugu Nancy, mie najua dhamani ya ndugu. Niliolewa 2009. nilikuwa nna marafiki msururu, ila kwenye harusi yangu nilijua tofauti ya ndugu na rafiki. Ofoucrse rafiki zangu walijitoa sana , kwenye bridal shower na send off ila ndugu zangu walijitioa mara elfu 10. Wengine hawakutoa hata mchango ila walijitoa mpaka nikaona ni mchango mkubwa sana, ndugu mpaka upande wa mamangu imagine na mie sikulelewa upande wa mama, ila ndugu za mama yangu walikuja kusaidia from day 1. Na pale ndo nilipojua dhamani ya ndugu, kwa kweli walinistiriiiiiiii. Na ningekuwa mtu wa kuishi kwa kuthamini mashoga tu nasahau ndugu labda ningeishia kufanya harusi kama ya JACKIE BEACH BABE. Harusi ya mashosti tuuu, ndugu noo,,,,lol…

Nancy wewe umeshakuwa kioo cha jamiii, hutakiwi kuishi hivi na ndugu yako wa damu,

Anyways, Nancy I hope you won’t hate me. Na hata kama ukinichukia as long as ukipatana na dada yako mimi naona mission accomplished….

PS: COMMENTS ZA KIZUSHI HAZITORUSHWAAAA….WEKA COMMENTS ZA KUJENGA SIJAWEKA HII POSTI ILI KUMWANIKA NANCY AU DADAKE….

Read More

DADA WA DIAMOND AONA WIVU MUMEWE KUFATANA NA BOSI WAKE…..LOL..

Juzi kati dada wa Diamond ,Esma aliposti video hii ya Diamond na Zari wakiwa kwenye malovey dovey jikoni

na kuweka harsh tag ya utata

Hashtag ilisoma  #mapenzikupetipetisiowapenziwetusiekutwakiguunanjiakumgandamtu

Kama ulipitwa na video bonyeza hapa….Ila muwaache na sufuria zao

Hash tag ni hiyo…..Ofcourse hashtag iliibua balaa huko insta….

Mweeeeh, yamekuwa hayo tena…hahahha

Ofcourse team Wema walivamia ikabidi afute hiyo hash tag haraka sana….lol..

Team Wema jamani, ukiambiwa wengine hawajawahi hata kumuona Wema hutoamini…..

Kuna ule msemo unasema “mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe”

Huyu aunty  mumewe si ni mfanyakazi wa Wema sasa alitaka akamgande nani kwa mfano??? Yaonyesha huko ndani kwake hakuna amani kabisa yani,

maana mwanamke mpaka akiamua kuanika matatizo ya ndoa yake hadharani ujue kimenukaaaaaa…..

Ila labda mngempa kitchen party jamani, ndoa zote zina matatizo yake,hata wake za wazungu hapa kuna siku tunalala mzungu wa nne na waume zetu au kwa pande hizi mambo ya kupigwa exhale to the couch for a few days…. Ila hakuna mwanamke mwenye kuijali ndoa yake anaweza aanika matatizo ya ndoa yake hadharani maana chances are mtapatana tu,sasa imagine mmepatana alafu watu ndo kwanza wanawachora……

Mdau we unaonaje? au ndo uzungu umezidi??? hahahhaha,maana wanawake wa kibongo kwa kuvumila matatizo sasa sijaelewa

Ila huyu dada kachekesha aisee, kama kweli anampenda mumewe si amtafutie kazi kwa kakake  ili aachane na madam, maana familia yao inapata tabu sana ,yani wanajiumiza sana kisa PETIT kuwa mfanyakazi wa Endeless Fame. Kama kaka yake kweli anampenda dadake kuliko kumnyali shemeji yake ni bora ampe kazi awe anamfata yeye.. hahaha,haki ya nani dunia hii, kweli fanya Wema uende zako…. Hivi mtu unaanzaje kuona wivu mumeo kufatana na mtu ambae ndo aliwaonganisha na kussuport mapenzi yenu from day one…. Mmmmh…… Alafu sasa analalamika tuu kama anaweza si amtafutie mumewe kazi ingine kama Petit akikataa kazi ingine hapo kweli ana haki ya kuwa na wivu kuwa alimtafutia dili lingine ila Petit yeye bado anataka kufatana na Wema tuu….

Alafu hivi mmenotice kuwa kwenye familia ikitokea wooooote ni maskini ila mmoja tu ndo anakitu huyo mmoja mtamnyenyekea hata kama yeye hana time…Huyu dada jinsi alivyo support mapenzi ya kakake daily ila kaolewa kakake kashindwa hata kutoa hongera kwake kwa mumewe ,dadake kazaa kashindwa hata kumpa hongera ila mnenguaji wake kazaa katoa hongera alafu huyu Esma badoo tu anamnyeyekea kakake na kurusha ma video zake,etc. kha! Kweli pesa kitu kingineeee,hahahahhaha….Im sure na yeye angekuwa na pesa zake angechuna kimyaa mpaka Diamond nae ajifunze kumsupport dadake…. Mwenzie alichukiwa kona zote kwa kuwa close na mawifi wapya kutwa ila kaka mtu shemeji mmoja tu kashindwa kumu accept…Mweeeh…..Jamani somesheni ndugu zenu muinuke woooote maana akinuka mmooja inabidi wote mumsujudie….

PS: VIPI MMESHA CALM DOWN???? HAHAHHAHAHA

Read More

MNANIONEA BUREEEE……

Mweeeh, sasa naona natumiwa na waoga waliotaka kusema nilichosema ila wanaogopa so wanafikisha message zao kwa muhusika kwa kunitoa mimi kafara….hahahaha

Jamani, mmenitukana sana leo matusi mazito mengine nimeshindwa kurusha comment.

MMENIITA MNAFKI, sijui nini kila kitu eti kisa nimesema nimeamua kuacha kuongea mabaya juu ya CCM, wabunge wake na wagombea urais wake.

Wengi wamedhani eti nimejitoa katika vita sababu eti nimenunuliwa  au nimetishiwa …. sijatishiwa na mtu yoyote  na wala sina mtu nnae mwogopa dunia hii zaidi ya Mungu . Siwezi kumuogopa binadamu eti sababu ana pesa au sababu ana power nchini kwangu,yeye sio Mungu, binadamu hawezi kunifanya lolote lile. Ntakufa siku Mungu aliyonipangia sio siku binadamu atakayotaka….

Naomba kurudia tena, nimeamua kuachana na hii vita dhidi wya viongozi feki wa Tanzania sababu kuna issue imeibuka jana ambayo imeibua isssue ya conflict of interest. So I have to stay away……

Nimeumizwa sana na matusi yenu fans wangu pamoja na wasomaji wangu, yani kweli mpaka leo hamjanijua mimi ni mtu wa namna gani? Kweli mimi ni mtu wa kununuliwa au kuogopeshwa????? Sina utajiri mkubwa ila ALhamdulliah maisha yangu yanaridhisha, nimesoma nna elimu nzuri najua kuhangaika na nina mume anaejua majukumu ya kulea familia. Sina shida ndogo ndogo kiasi kwamba ntaacha utu sababu ya pesa. Sina tamaa ya pesa na sitakaa kuja kuwa na tamaa ya pesa sababu nimelelewa kwenye pesa, nimekulia kwenye pesa, naijua pesa so hainistui kabisa yani….

So nawaomba tena kwa mara ya mwisho, naomba muwe patient naomba mue wa subra wapenzi wangu…mTakuja kuelewa kwanini nimechana na hii vita….

Mimi na nyie tuko same side…..Sijahama team. Im still team ukweli na uwazi…… ILA limekuja swala la conflict of interest …..Its just not ethical for me as a blogger to continue this war….

Pia nimeshangaa sana watu wa Chadema wananichamba eti traitor, Chadema mnikomeeeeee kabisa mimi sio Chadema supporter mimi ni mwana CCM toka nimezaliwa mpaka leo na sijawahi kusema sikipendi chama changu sasa nashangaa mnataka kunitumia mimi kupigana na ccm , mimi siko against CCM mimi niko against  vitendo vya viongozi wengiii wa ccm hususan hawa waliopitisha SHUT UP TANZANIA LAW. PAMOJA NA MAFISADI…

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDU (BILA MABEPARI WA SHUT-UP TANZANIA LAW NA MAFISADI)……

“Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai.  Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma  tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa  kwa ugoni Kaisari  akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope  halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.”  – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere,

Kama BABA WA TAIFA , Nyerere alimkataa mwaka 1995 kwanini sisi vijukuu wa Nyerere tumkubali 2015???…..Ni nini kilichobadilika toka 1995 mpaka 2015 zaidi ya matukio ya kuprove Nyerere was right in 1995?  #Richmond

KWAHERINI

PS: NAOMBA TUENDELEE NA STORY ZA KINA DIAMOND NA MIMBA YA ZARI HUMU NDANI NA TUACHANE NA MAMBO YA SIASA…PLEASE MTANIELEWA BAADAE, TRUST ME. SIJAFANYA KILE MNACHODHANI NIMEFANYA…. ILA IMEBIDI NITUMIE BUSARA , NA NYIE BAADAE MTANI SUPPORT KWA HILI……NAOMBA TUWE PATIENT….

Read More

LE TAMKOZZZZ ……………

Wapenzi kuna habari nimezipata leo hii ambazo kwa kweli zimenifanya niache kuwa attack CCM na wagombea wao wa urais.  Hapana sijatishwa Wala kununuliwa na mtu yoyote yule. Ila imebidi nichukue uamuzi huu kutokana issue ya conflict of interest na kwamba naona Nikiendelea na hii vita huko mbeleni ntaonekana ni mnafki.

Kama mjuanvyo mimi ni mwana CCM wa damu. Ccm Iko damuni mwangu so naomba ieleweke Kuwa yote niliyoyasema humu niliyasema kwa uchungu mkubwa na mapenzi kwa nchi yangu na chama changu na sababu hizo hizo za mapenzi na nchi yangu ndo zilizonifanya niache kuwajadili wagombea urais wa CCM…

Although taarifa hiZi zimenifanya niachane na mpambano huu dhidi ya ccm na wagombea urais wake ila pia taarifa Hizi zimenifariji na kunipa hope kubwa mno na Chama changu. Soon mtanielewa. Yani kuanzia leo nalala usingizi mnono najua one day kila kitu kitakwenda sawa. Please msichukie wala kuniona traitor very soon mtanielewa na kunipongeza kwa msimamo huu. 

Kama mnavyonijua mimi sipendi unafki wala uonevu na soon mtajua Kuwa hizi principles mbili ndo zilizonifanya nichukue uamuzi huu mgumu.   Kidumu Chama cha mapinduzi

PS: Nawaomba muwe na subira wapenzi, pls vuteni subra soon mtaelewa na naamini mtaona busara yangu kwa kuchukua uamuzi huu…Yes nimeedit maneno makali niliyoyatumia kwenye posti za nyumba

Read More

VITA DHIDI YA SHUT-UP LAW – MENGI NA ROSTAM AZIZ WAKUMBATIANA……

 

Kimenukaaaaaaa, mpaka Mengi na Rostam wamekumbatiana katika kuongeza nguvu ya kuipinga shutup law…..

Unaambiwa hivi the enermy of my enermy is my friend….lol……

Ndo maana mie nilikuwa nawashangaa mburulaz wanaosupport shut-up law eti kisa Mange haisupport na wakati na yeye mwenyewe 

ni victim wa shut-up law….Ona watu wanaojua kutafuta pesa na kulinda maslahi ya biashara zao wameona bora wapatane ili waongeze nguvu za kupigana na adui…..

Read More
1 2 3 148
Designed by muzemultimedia web design Tanzania