WEMA SEPETU – IN MY SHOES S02EP13

Nipo busy kidogo nikitafuta pesa… Embu burudikeni na mtoto Sepetu kwanza wakati nahenyeka…..

PS: Alafu mambo ya C’s mum mngeacha maana nachoka block comment… Jamani mbona yameshaisha…Ndugu wa baba mmoja tu huzozana itakuwa mie na C’mum…. Mbona kina KOKU wananiwekaga sawa nikikosea na tunaendelea na maisha???? C’S mum mtu wangu wa long time. Alafu si mnajua nilikuwa nna stress sana kikawaida nisingelipuka vile… Anyways, like I said freedom of speech ipo pale pale, kosoa mtu unavyojisikia ila tusivuke mipaka tu…..Ama nene!!!!

 

 

 

 

 

Read More

MAMBO YA ENTOURAGE – SWAGGA MPYA ZA DIAMOND

Naomba nianze kwa kusema kuwa Im not a hater….. Naandika kama blogger tu sio hater….

Ni maoni yangu tu kama Mtanzania na katika kumpa ushauri kijana wetu….

Anyways,wewe kama mtanzania unaonaje hizi swagga mpya za Diamona kusafiri au kufatwa nyuma na kundi la watu wakiwemo mameneja wake, ndugu,mpiga picha, etc….

Kwa maoni yangu naona kama mameneja wake wanampoteza tu. Itakuwa kaambiwa akitaka kuonekana ni big star basi lazma awe anafatwa nyuma na kundi la watu everywhere he goes.,,,,,

Nimemuelewa kidogo sababu labda kaona mastaa wakubwa wakubwa duniani huwa wanakuwaga na entourage kubwa ya watu ila jamani they can afford kuwa na watu wote wale… Some of them make over 10million dollars a year sasa kulipa watu wote hao kumfata fata ni pocket change kwake. Tayari wana utajiri ambao hata wajukuu zao watakuja kuukuta ,wana majumba in every city wengine mpaka Palm Jumeirah Dubai wana mavacation home sasa huyu kijana wetu ambae mpaka leo bado anaishi kwenye nyumba ya kupanga kwanini analipa watu kumfata fata nyuma hivi? wakati it’s very unnecessary.

Hvi whats the point of mameneja wake kumfata fata kila anaposafiri? Ndugu yake Romy Jones its okay kumfata fata, wata kuwa wanaenjoy ku hang out together all the time so anaona poa kumkatia ticket asafiri nae. Ila kwa uDJ mmmh? Hivi T.I alivyokujaga fiesta alikujaga na DJ wake?? labda mie mshamba sielewi…lol.. Aseme tu anaependa kusafiri na ndugu yake coz they are very close.

Madansa wake ndio wana ulazima ila hao wengine ni show off ambazo zinamrudisha nyuma….

WOOOOOTE TISA KUMI NI MPIGA PICHA ALIEMWAJIRI FULL TIME kumfata fata everywhere….

Uwiiiii, kweli only in bongo… Na huyo official photographer ni wa kumfata kumpiga picha za kuweka instagram haahahahahhahaha…

Jamani wenzenu mastaa wa majuu wakiwa mastaa hwana haja ya ku kulipa photographer, mapaparazi wenyewe wanakimbizana kila kona kukupiga picha,na kama swala ni quality photos ukiingia online 5 mins utapata picha zako zooote ulizopigwa na media kwa siku hiyo. Wenzenu huku wakitaka kuwa kwenye news  wanawatip off media where they will and what time alafu media wakifika wanajifanya kushtuka sasa na huyu kwa ustaa wake shingongo anatakiwa alipe wafanyakazi wa kwenda hadi zanzibar kumpiga picha Diamond. Ila sasa anamrahisishia kazi maana picha zote zipo instagram anazilipia mwenywe…hahahahahha….KWELI akili ni nywele….

Imagine afanye show, then alipe kila mtu hapo, hivi kweli atafika mbali financially huyu kijana?

Haya maisha anayoishi wanafanya mastaa ambao wana hela mpaka hawawezi tena kuhesabu, yani wameshajenga maisha yao mpaka ya miaka 20 ijayo

sas ahuyu kijana wetu jamani nyumba yake tu bado hajamaliza hizi show off za hivi za nini?

Kila mtu anajua he is big now, he doesnt need to spend money kufatwa fatwa na watu for people to know that…..

Naomba kuuliza hivi ni mara ngapi tunakutana na mastaa wakubwa huku marekani wako public places hawana mabodyguard wala nini????

Nilishamuona Usher mall ila kwa mbaliii  anahang out  na demu wake ukiambiwa ni superstar huamini, hivi kwani hawezi eka bodyguard wa kumfata fata muda wote??

sasa kaka etu hata romantic getaways yeye anafatana na bodyguard na wapiga picha…hahhahahhahaha

Hahhahahahahhahahahhaha……Haki vile….. IMAGINE hapa anawalipia watu wooote hao hotel rooms, na kuwalisha wooooooote ,na ticket za ndege juu hapo bado hajawalipa mishahara… HIVI kijana ana future yoyote huyu kweli? Ningeelewa kama angespend pesa zake kulipa wasanii wakubwa wakubwa kufanya nae collabo kama alivyofanya kwa Davido ila sio kwa picha za kuweka instagram….

Im not a hater jamani, ila sometimes unajua bloggers tukiongea muhusika akasoma hata kama hatopenda ila inamsaidia na atabadilika…

Hivi jamani hii romantic getaway niambie still kabeba wafanyakazi wooote, na wote wakavalishwa white ili picha zipendeze…haahhahahahha

 Nangoja siku nione beyonce na jay Z wako vacation na wafanyakazi wako ,wapiga picha wao ,mabodygurd wame color coordinate nguo zao ili picha zipendeze….

Alafu sasa kapata na mwanamke ambae na yeye ni mpenda mapicha na mashow off so hana hata wa kumshauri maskini…..

Sasa sijui ndo mpiga piha inabidi aamke asubuhi aende chumbani kwa bosi na mke wake wavae ma bathrobe yao awapige picha wanakiss then warushe instagram?hahahahhaha

Duh, kazi kweli kweli….. Kama kuna mtu amewaambia kuwa mastaa wa ulaya ndo wanafanya hivi kamdanganya jamani wenzao wanaviziwa na paparazi tena picha zinakuwa hazina quality sababu ni za mbali mnoooooo. Ukiwa star huna haja ya kufanya yote haya media watauwana kutaka picha zako…

ALafu pia management yake wangemwambia kuwa sometimes wasiwape mashabiki everything they want to see. Keep people curious. HAPo ndo mashabiki wanakuwa na hamu ya kukujua undani wako sasa hawa kila dakika 5 picha soon watu watawachoka kabisaaaa

kama mimi ,mwanzo nilikuwa nawaona hot news kila siku lazma niwaandike ila mpaka habari ikaboa wasomaji wakagoma coz its too much.

Yani anaewadanganya hawa kuwa mastaa wa mbelez ndo wako hivi sijuiii…

Hivi hata hao wanaigeria kina Davido sijui PSquare hivi huwa wanafanya any of this stuff??? Ndo maana wanamuziki wetu huwa hawawezi kumaintain status muda mrefu ni sababu wana loose focus. Yani watanzania alietupa laana yakushow off sijui ni nani… hahahahhaha… Yani tuko tayari kuspend hata last senti kwenye account ili mradi ushow off.

I hope ataichukulia hii vizuri na kubadilisha hili….

Bado ana safari ndefu sana huyu kijana. Hizi pesa anazochezea sababu ya picha za instagram atakuja kuzikumbuka sana later. Hao watu anaowakatia maticket kumfata fata nyuma for no good reason atakuja kuzikumbuka. I know for a fact hakuna mtu anaemlipa kwenda kufanya show akampa na budget ya mpiga picha wake, ya dj wake, ya mameneja wake na ya GF wake. Navyojua kwenye show anapewa budget yake na wacheza show wake.PERIOD……Hao wengine ni yeye inabidi awalipe….

UPDATE….

Mweeeh,haya one of Diamond’s managers amenishushuajeee sasa???????

OMG, Is he for real? jamani si niliwaambia Diamond itakuwa kaambiwa na ma manager wake kuwa kufatwa vile na kundi la watu ndo ataonekana kama big stars wa marekani??? Oneni jibu la manager wake jamani…. Oneno mfano alionipa??? OMG, Yani nimeishiwa nguvu zooooooooote…. Yani nimeishiwa na maneno yooooooooote. Nimeambiwa I know nothing about ent business nikamgoogle LADY GAGA nione alivyo na entourage kubwa ndo niongee…NGACHOKA!!!! Yani nimekosa hata la kumjibu kuhusu lady gaga kama wewe unajibu etu tusaidie pls…

Yani la LADY GAGA limenimaliza sina hata la kuongeza, Hivi huyu manager amelewa au yupo sawa? hivi kweli anajustiy spending ya Diamond kwa kucompare na spending ya artist ambae in 2013 alimake $80 million, pesa ambayo hata kuiandika kwa tsh siwezi maana ntaandika masifuri mpaka nidate, pesa ambayo mpaka Diamond anakufa atakuwa hajawahi kuiona kwenye account yake,, hiyo pesa LADY GAGA kamake in 1 yr jamani na ni pesa ambayo diamond mpaka anakufa hatoishika mkononi alafu ndo mtu kama huyo wanageza swaga zake, si bora wangesema wanamgeza Neyo au Ray Jay mdogo wake Brandi kidogo pesa zao labda Diamond anaweza kujikuna kuna akafananishwa nao. NGACHOKAAAAAAAA……hahahahhahahahah,,

Alafu huyu manager inaonekana anapenda shari alafu sasa ni mwanaume ..Mie sikuongea vibaya nilitoa ushauri hata yeye angeweza kujibu kistaarabu kwa kuweka  hoja za maana sio mambo ya kusema natafuta KIKI or sijui na mie nataka kujoing entourage yao…Kha.. Although wewe unajua kila kitu kuhusu ent business let me tell you kazi ya kubishana na bloggers juu ya Diamond ni kazi ya publicist wake sio kazi yako wewe, so labda ungepunguza mmoja wa mabeba mabegi ya diamond hapo mkamuwekea na publicist kama LADY GAGA….hahahahhahahahhhahahaha…….

Anyways, sina hata cha kuongea maana jibu lako tu limedhihirisha kuwa huna akili hata moja na umesha prove my point kuwa wewe na hao managers wengine ndo mnaomdanganya Diamond. Ila siku ustaa wake ukiisha na pesa zikakauka tunaomba muendelee kumfata fata nyuma hivyo hivyo sio mumkimbie….

Unasema na mie mtanilipa niwe naandika habari za Diamond, sasa kama Diamond kashindwa kukulipa wewe pesa ya maana mpaka mkeo- ESMA amekukimbia kwa  kuchoka maisha ya kubadilisha mboga ndo ataweza kunilipa mimi ??? Mke alikuwa anataka umnunulie Range Rover akakuta mume kumnunulia  Suzuki tu hawezi…hahahhahahahah……Sasa mie mtanilipa nini????hahahahahhaha

Again niliongea vizuri na kusema I hope Diamond ataichukulia vizuri nilisahau kusema I hope manangers pia wataichukulia vizuri.lol… Haikuwa nia yangu kuamsha vagi huko instagram.  Good thing is angalau tumejua ujumbe umefika vizuri kwa wahusika  na hata Diamond akipitia comments za fans wake ataona mawazo yao na nnaamini hata kama atafanya ubishi ila lazma atakuwa anafikiria mara mbili mbili hili na kuna siku ataanza kufikiria ya mbele yasije kumkuta ya Mr. Nice au Saida Karoli, mwanamuziki ambae nyimbo zake  mpaka leo hii zinapigwa ndani ya big movies za hollywood na hana hata shingi mia moja benki nadhani aliuzaga hata rights za huo wimbo wake kwa milioni 2 labda…hahahhahaah…Hii yote inatokana  na mwanamuziki kuzungukwa na mburulaz kama wewe Salaam…….Yani kwa jibu ulilotoa inatosha kuonyesha watanzania in 5-10 YRS time Diamond atakuwa wapi career wise.

Read More

MY DAUGHTER IS AN A-STUDENT……..

Nguo nilichagulia na Bhoke ,hahahahha eti alikuwa anataka mamake awe the coolest mom kwenye event….hahahahaha……

Yani nikiwa naenda kwenye mambo yake naacha anivalishe maana nisije mwaibisha…hahahhahaha

I love this denim on demin look…..

Jukwaa hilo…Hapo mama mtu mchecheeeee nasubiria mwanangu apande…hahaha

Jamani askwambia mtu kama mzazi hakuna kitu kinakupa furaha na matumaini kama kuona mtoto wako anafanya vizuri shuleni jamani….

Sio kufanya vizuri tu,yani anafanya vizuri kupita kiasi mpaka shule wanam recognize…….

Mtu na mommy ake… mwanangu mrefuje sasa….lol..

Mommy’s shoe game…

Jamani I don’t remember the last I was this excited about anything or the last time I was this proud of anyone , including myself….

Yani leo mama mtu bichwa hilooooooo….hahahhahhaha……..

Bhoke alinipiga mkwala kuwa nikipigia vigelele atasema hanijui…hahahahhahahahahhah……

Nkasema poa basi ntashangilia kwa kizungu…hahahahha

UPDATE:

I guess kuna wengine ambao mpaka leo hawajui the kind of mom I am. Yani mie niko tayari nisipendeze ila niwanunulie wanangu pamba za ukweee…

Chaumbea hapo aliesema mama mtu nikajinunulia mwenyewe kiatu nikamsahau mwenywe shughuli yake…hahahahha…..

Her shoes are more expensive than than mine just so you know…. She was wearing JORDAN’S .. Hiy0 shule yao wanavaa uniforms so mchezo wote wanamalizi kwenye viatu, wanataka branded sneakers….lol….Hapa nadaiwa timberlands za kuvaa shule ndo zawadi yake ya kufanya vizuri….lol….

Atleast she is still into sneakers,uwiii siku nikianza ombwa high heels ntajutaaaaaaa……hahahahhahaha….

Read More

NISHAURINI – MAJI YAMEZIDI UNGA….

SHAURINI MWENZENU MAJI YAMEZIDI UNGA..
Nivumilieni gazeti langu. mimi ni mdada wa miaka 27yrs kwetu tuko wa3. mimi na kaka zangu. mama yetu alishakufa since i was 3yrs old. Mungu alivyomwema akatupa step mother mzuri mnooo mama yetu wa kambo katulea toka na miaka 7 mpaka leo. ni mama yangu na tunampenda kufaaa!!! baba ni mfanyabiashara mkubwa hapa mjini nashukuru Mungu kwa maisha yetu. baba ni mtu wa totoz. haya ndoa ya baba na mama ni ya misuko suko na kuvumiliana,si unajua wanaume wakiwa na hela,tabu tupu!!! baba akaanza kuruka na shangingi mmoja mtangazaji wa ITV. huyu mdada aliolewa na kaachika na ana mtoto mmoja. toka baba ameanza uhusiano na shangingi huyu, ndoa ya baba na mama ni kwisheni.. kila siku mama anakula ngumi bila sababu,mama yangu anatoka manundu kisa baba anamwanamke mwingine wa nje. 2weeks ago baba kamfukuza mama yetu nyumbani na mimi nikamwambia mama aje kukaa kwangu.. shangingi wa ITV kahamia nyumbani kwetu na mafurushi yake yote..msichana wa kazi nyumbani akanipigia simu kunipa umbea kwamba shangingi kaingia ndani na nguo zake! nilipatwa na hasira nikatoka kazini jioni nikapitia nyumbani nikawaita wahuni wa mtaani kwenu wangie ndani wamchape viboko yule shangingi kwa kuingilia ndoa ya wazazi wangu.. vijana wakafanya kweli,tandika viboko vya kufa mtu na mimi nikishuhudia. nikawa narecodi na mapicha kibao nikapiga ya ushahidi.
baba karudi kaambiwa kilichotokea,kanipigia kupiga marufuku nisikanyage nyumbani kwake tena. jamaniii huyu mzee wangu kama kalogwa vile! nampigia simu kujitetea hapokei anaishia kunitumia messeji eti nisimsumbue na hataki kuniona.
Mama yangu ni mtu wa kusali na kuomba sana,kama makanisa kamaliza yote kuzunguka na kuomba. mimi kama mtoto wa kike wa nimeshachoka na kuvumilia vya kutosha kuona jinsi mama yangu anavyoteswa na kuzalilishwa in the name of ndoa and keep the peace at all cost!!!! i wish mama yangu angekua na ujasiri wa kumwacha mzee wangu for good. mama yangu kateseka sana jamni,acheni tuu. sitaki hata kusikia kitu kinachoitwa NDOA.USHENZI MTUPU!!

WADAU KWANI NIMEKOSEA KUMTETEA MAMA YANGU JAMANI???

Yes ile section yetu ya kutoa ushauri na kushare life experiences imerudi tena….

kama ungependa kuomba ushauri, kutoa kero yako, au lolote lile  nasi tuma email kwenda kimambimange@gmail.com

Read More

HOT NEWS: OMMY DIMPOZ ARUDISHIWA AIRPORT USA+ WEMA & IVAN – IT’S VERY ON……..

Ommy Dimpoz alikuwa ana show ya Valentine kwenye mji wa Las Vegas lakini immigration walimkatalia kuingia nchia marekani na kumrudisha Tanzania on the very next flight.

Ommy Dimpozi alirusha picha insta akiwa transit kwenye mji wa Amsterdam na baada ya hapo ikawa kimya ndo watu wakafatilia na kuwasalinia na promoters wake wa marekani na ndo habari ilipotoka…

Nimejifunza kitu kimoja hapa, ukiwa unaenda nchi kubwa kubwa zenye immigration za utata kama marekani, Canada, Uk etc usiweke picha insta mpaka utakapopita immigration….Seriously… Maana kama Ommy asingerusha hizi picha za safari sidhani kama wambea wangemfatilia sana….

Pole sana Ommy, usijali tengeneza tu mambo vizuri watakupa visa tena……

BTWN OMMY DIMPOZ IS MY FAV TZ ARTIST…..

In other news, Tanzania’s sweetheart ,Wema Sepetu is officially dating mheshimiwa Ivan kutoka Uganda ambae kwa sasa anaishi South Africa.

Kwa msiomfahamu IVAN ni ex-husband wa GF wa Tanzania’s superstar Diamond PLATNUMZ anaejulikana kama Zari the boss lady…..

Yes, this is 120% confirmed,no, its 200% CONFIRMED. Kwasasa hawataki kuweka relationship yao out there kama kina fulani sababu wao wako pamoja sababu wanapendana na sio sababu wanataka kushindana na their exes au sababu they are looking for attention. I think Wema kajifunza kuwa hizi relationship za mapicha kila baada ya  dakika 5 huwa hazi last so kaamua yeye na Ivan mapenzi yao yawe ya kwao wao mpaka hapo watakapo ona wamejuana vizuri ndo watayaweka wazi…

Yes, wengi wataona kuwa sio sawa hawa kuwa pamoja kwa sababu zilizo wazi ila pia mkumbuke kuwa sometimes watu hukutana kwenye circumstances za ajabu ajabu. Yes,labda wasingejuana kama sio exes wao kutoka pamoja ila again labda ndo ilikuwa njia ya Mungu kuwakutanisha wawili hawa….Hata Rihanna aliimba ” We found love in a hopeless place”  naongea hivi sababu, it is real btween these 2 na wanapendana haswaaaa. Na nimeamua kuwa support mapenzi yao sababu wanayaficha which means ni mapenzi ya kweli,sio mapenzi ya magazeti au kuonyesha watu au kutafuta attention like kina fundenge… Yani ni mapenzi ya kiutu uzima sio ya nursery school. Nimeyapenda mnoooo… Na mdogo wangu mnamjua kwa kufall in love…… Hahahahahahaha……

Also Im sure utakuwa umenotice hiyo DP kwenye insta ya wema hiyo ya Lipstick ni kwamba Wema analeta lipstic za maana zenye jina lake, in each and every color… Na project nzima iko funded na mzee mzima Ivan…. STAY TUNED……

Haya ndo mapenzi mazuri sasa…..Ukimpenda mwanamke unamnyanyua ili na yeye aweze kujitegemea na awe your equal.. Na mwanamke pia akiwa na mwanaume anaemnyanyua hivi atampendaje sasa? Yani mwanaume utafurahi maisha mbona…. 

Anyways, siku hii news ya Wema and IVAN iki break out officially,just remember where you heard it first… hahahahhahaa

So,yes, Wema na Dimpoz hakuna kitu chochote kinachoendelea, Walikuwa wanafanya music video,basi… Ila wana enjoy jinsi wanavyowazingua na mapicha na ku divert attention from the real couple….hahahaha…

Alafu naskia King Larence kapigwa mkwala wa hatari na Ivan not to say  or publish any pics ya relationship yake na Wema….Jamani ndo maana siku zile wakati King anamdhalilisha Zari nilikuwa nawaambiwa kuwa dont blame King, King anafanya vile anavyotumwa na IVan, nothing more, nothing less. Mbona issue ya Wema kaambiwa aache na kaacha?????hahahahahha……..

Mmmh, ona Ivan na Wema wanavyozuga watu huko instagram. Wema anacomment kwenye picha za Ivan na Ivan ane anamjibu kama vile hawajuani…hahahahahhhahahahhah

Read More

HOW WAS YOUR VALENTINE’S DAY???

Haya wapenzi…

Eti V-day ilikuwajeeeeee????? leteni mastory na maumbeazzzz…

Vipi hubby/mpenzi alikutoa au alikukimbia? Na ma side chic vipi mliwaona waume za watu au walikuwa kwa wake zao?

Wenye ndoa za ukweli zisizo na drama mume alikufurahijeee???

Tunaomba wote musheeee, kuanzia wake mpaka ma side chics…..lol…

Mie I didn’t have much of a V-day…. Nilikuwa home (Los Angeles) na watoto siku nzima…….

Haya mliokula raha za v-day leteni mambo…

Read More

LADY JAYDEE AELEZA SABABU ZA KUMUACHA MUME WAKE, GADNA…..

Jide ameamua kufunguka kupitia page yake ya Instagram na kueleza mashabiki wake kwanini ameachana na mumewe 

wa zaidi ya miaka 10. Gadna G. Habash…….

Duh, kweli kina ndoa ina mambo yake ya ndani ambayo watu hawayajui….

Ila wanaume jamani sijui wana problem gani, una mke anaetengeneza pesa, kajenga nyumba mnayoishi ila bado unamkosea heshima na kumdunda juu….Inaumaje sasa???? Ila mie jamani bora mwanaume anifanyie yooooote but not kipigo,uwiiii siwezi vumilia kupigwa jamani.Kha! Na nna bahati maishani sijawahi pata mwanaume mpigaji  zaidi ya zamaniii kuchapwa bao moja tu mwanaume,  uwiiiii nilikimbiaje polisi sasa???? hahahaha….

Sijaelewa hiyo part aliosema kuwa kaondoka nyumbani bila kuaga na hajarudi tena nyumbani sasa ni kwamba ile nyumba kaamua kumwachia mume au watauza wagawane baadae? Duh….Noma…

Gadna nampendaga sana huwa ni mtaratibu na mstaarabu sanaaaaa yani nimeshangaa kuwa ana tabia hizi.Duh…..Ila sasa ataishije mjini si atachoka sana bila Jide. Au we mdau unaonaje?????

Wanawake wa Tanzania embu fateni mfano wa JIDE acheni kuogopa divorce jamani. If you are not happy chapa lapaaaaa, eti utachekwa umechika. Acha wacheke, siku uki settle na anaekuheshimu na kukupenda na wewe unampenda and you are HAPPY wewe ndo utawacheka wao.He who laughs last,laughs best. Hukuletwa duniani kuteseka kwenye ndoa ili ufurahishe watu ambao hawakulishi wala kukuvisha…. 

BONYEZA HAPA Kusoma habari vizuri na kusoma comments za mashabiki wa Jide 

Read More

VALENTINE’S DAY HIYOOOOO….. NANI ANAPENDWA ZAIDI??? HAHAHHAA

Uwiiii chezea uke wenza wewe….

Haya jamani Valentine’s day ndo hiyooooooooo….

Unajua hiyo siku ndo huwa mtu unajua mumeo au mpenzi wako anakupenda wewe zaidi au mke mwenzio zaidi….

Ukweli ni kwamba wanawake kibao wako na wanaume ambao wanajua either ana mke au kama hawajaoana wanajua kabisa BF wangu  ana GF mwingine ila unajipa moyo kuwa  wewe ndo unaependwa zaidi na kuwa Valentine’s day ndo haswaaa siku ambayo yakujua vizuri….

Je atatoka na wewe au atatoka na mwenzio???Hahaha… Ila wanaume wajanja hii pia wanaweza kupindisha so be careful jamani….

Hii imenikumbusha valentine’s flani hivi wakati nipo chuo,nilikuwa nakaa Mabibo hostel…. Okay, bwana we have all made our mistakes huko nyuma…. Mnajua nilikuwa nasoma kwa Mugabe huko kuanzia form 1. So by the time naingia mabibo hostel nilikuwa sijui chochote kuhusu Dar au kumjua mtu yoyote yule. Nikajikuta namdate jamaa flani hivi, alikuwa hajatulia hata robo ila mie nilikuwa simjui wala na alietu introduce nae sijui alipewa hela maana hakuniambia kuwa jamaa alikuwa ameoa….lol…

By the time mie nakuja kufind out jamaa ana mke ni months later… Ila jamaa alikuwa very successful, mzuriiii, kijana, yani akisema hajaoa hubishi…… Basi bwana ikaja Valentine’s day,mpaka hapo nishajua kaoa ila sasa nafanyajeee. Basi jamaa alivyomjanja, akasema ana work a bit late ila lazma anitoe. Kweli bwana by saa 4 huyo mpaka mabibo hostel nkapelekwa dinner. Nkawa najiambia mwenyewe huyu kweli kamchoka mkewe,leo kamkimbiaje kwa mfano?? au kama vipi kanifia kishenzii…lol.. Kumbe bwana jamaa ana akili kushinda zangu…hahahahahaha…. Kumbe bwana jamaa alienda  dinner na mkewe saa moja hivi pale Serena, alivyomaliza dinner na mkewe ndo huyoooo mpaka chuo kunitoa mimi out….hahahahaa……Nikaja kujua about a week later baada ya mtu kuniambia alimwona Serena dinner on Valentine’s day ,nkawa namsbishia namwambia hapana hakufika huko VALENTINE’S day bwana. Tulienda  Kawe huko for dinner. Nilivyoambiwa mida aliyoonekana  na nguo alizokuwa amevaa mbona nilichokaaaaaaaaa mwenyewe…hahahhahha…

Uwiii jamani nikisema wanaume wa kibongo hawafai muwe mnanielewa…hahahhaha…Mie nawaogopaaaaa…..Acheni tu niwe muke ya Muzungu… Wabongo ni nomaaaaaaaaa…. Waongojeeee sasa…..hahahhahahaha….Yani ni ma professioal wa kucheat….

So jamani msidanganywe Valentine’s day. Mkamate mumeo/mpenzi wako kuanzia saa kumi jioni mpaka kesho yake la sivyo na wewe utachezewa huu mchezo. Utapelekwa dinner ya saa kumi na mbili jioni urudishwe home then ajifanye anaenda msibani kumbe anaenda dinner ya pili….hahahhaha

au wewe utakaepewa dinner date ya saa tatu usiku ikataeeee, ujue mwenzio anapelekwa dinner mapema zaidi then akimaliza ufatwe wewe. Then wote mjione mnapendwa zaidi kumbe hakuna hata anaependwa anawachezea akili tu….. hahahahhaha……

Jamani wanaume wa kibongo ni nomaaaaaaaa….. Kuna baba mmoja yeye kila mwanamke anampa birthday tofauti.So mwanamke anajiona yeye ndo anapendwa maana a birthday ya mume alikuwa nae yeye kumbe wala sio birthday yake ya ukweli. hahahhahahahahha…Uwiiii

Jamani Valentine’s day  ndo hiyooo tena na hivi inaangukia jumamosi usimwachie siku nzima maana asije mmpeleka mtu lunch alafu wewe ndo dinner…

Mkamate the whole day, hata kuosha gari nenda nae au mpe watoto aende nao… hahahaha..

Ambao hawawezi kuwatoroka watu wao ambao ambao wana wanawake wa pembeni wanaowaogopa na kuwapenda basi kama ana mwanamke wa pembeni atajaribu kutafuta ugomvi na wewe ili siku ya Valentine apate kisingizio kuwa mlikuwa mmegombana ndo maana hakukutoa out.. Usikubali ugomvi wowote ule, yani hata alianzishe baala gani mwambie wewe huelewi una akili kupita zake ,mwambie asubiri huo ugomvi aulete jumatatu…hahahha

KAMATA MWIZI MEEEEEIN….

PS: Bado tunashughulikia suala la reply kwenye comments. for now ukitaka kujibu kitu alichosema mtu copy comment yake yote then paste kwenye comment yake then chini yake ujibu…..

Read More

WANANGU WANANICHANGINYI……

Haya Kenzo anataka mamake abaki na kipilili huku dada mtu hataki mamake nikae na kipilipili…

Yani Bhoke hataki rafiki zake wanione bila wig au weaving jamani….. hahahahha

Tena afanya kusisitiza atiii ili nisije sahau nkaenda mwaibisha mbele ya shoga zake na kipilipili changu…..

Yani hawa watoot jamani…. Sasa sijui Keanu nae atataka niwe na hairstyle gani…lol..

Maana sasa sijui nimfurahishe BHOKE au Kenzo……

Ndo nkamkuta shule na huyo shogake alietaka kunimeet mama mtu wakinisubiri….

Ningeenda na kipilipili mwanangu angenunaje sasa….hahahahhahaha

Read More

NTAPIGAJE VIGELEGELE SASA…..

Uwiii, so today my baby, my first born, my only daughter kaniletea hiii barua from shuleni kwao….

Tarehe 20 kutakuwa na fuction ya kuwapa certificate za achievement wanafunzi woote waliopata GPA za 3.0 and above…Uwiii na mwanangu mie yumo humo ati…… Uwiii nimedata kiaina…hahaha…

Jamani hii ndo semester yake ya mwisho kabla hajaanza high school mwezi wa 9… Yani she is ending middle school with a BANG!!!

Yani leo nna raha sana nakabusuje muda wooote…. Uwii nahisi this weekend ntafilisika kwa kumspoil…hahhahahaha

Hiyo Tarehe 20 nahisi ntakuwa typical African woman huko shuleni kwao maana ntapigaje vigelele sasa akipanda kwa jukwaa kupokea certificate yake????

Yes ,my daughter is an A student…Jamana natamanije aendelee hivi hivi aje kupata college  scholarship anisevie pesa zangu mie jamani….lol…

Mungu ni Mwema daima,naamini ataendelea kufanya vizuri…. Yes, the kids from Africa anawakimbiza wamarekani shuleni toka day one ….Si mnakumbuka hata wakati tuko Florida alikuwaga anapata hizi academic awards

Elimu ya bongo wala sio mbaya at all jamani maana bhoke kwanza hakusoma hata class 4 akaja hapa akaingia 5 na bado anawakimbiza na ma awards anapata……

Read More

JAMANI MBONA WANATUCHANGINYI??

hahahah, pls nikumbusheni comedian wa bongo aliekuwaga anasema mnanichanginyi instead of mnanichanganya???hahhahaa

Umbea umenibana sana nimeshindwa kuvumilia jamani….

Hivi wewe umeielewa hii projekti ya hawa watu?? Kwanza nilipata migrane ya ajabu baada ya kuona mapicha ya Wema na Ommy Dimpoz..

Yani nilichukiaaaaaaaaaa mpaka…Ila sasa naanza kuhisi ni projekti tu ya video wanafanya…hahaha

Nilinunajeeeee jamani. Na haya mastress yangu basi ndo mnuno huoooo utasema yananihusu…hahahha

I mean as much as I love Ommy Dimpoz , you don’t go from Diamond to Ommy Dimpoz, you go from Diamond to DAVIDO…..I mean hutakiwi kurudi nyuma ila kusonga mbele…Inabidi ukiachana na mtu uwe na mtu ambae hata huyo ex wako akijua mwenyewe anasema kimya kimya “duh kumbe demu wangu alikuwa mkali eeeh? anachukuliwa na yule?”  Maana akikuona na mtu mjinga zaidi yake ataona uwiiii bora nimeachanna nae….hahahhaa

Haya angalia hiyo picha ya juu, walipopiga picha Wema na Ommy Dimpoz then cheki na hapa alipopiga King Lawrence….

Uwiiii, nimechoka kabisaaaaaaaa…. Hii projekti jamani ni vipi? mbona wanatuchanganya? Sasa ndo King Lawrence anataka tujue yupo na Wema  au??? NIMECHOKA KABISAAAAAAA….

Haya mara wameweka picha wapo club na huyu demu mwenye ushepu wake…….

Embu jaribu kuwaza if Ivan aanze kuchukua Wema??? mmmmmh!!! Sasa Zari si atapata shida maana Wema hatompa tena pocket money??? Imagine mtu ambae ulikuwa unatamba African nzima na ex wake mara ndo kawa GF wa ex wako anae kulisha na kukuvisha,uwiii si waweza pata kiwewe??? hahahaha… 

hahahahhaha, mie mmbea….lol…

Ila uwiiii I hope isitokeee jamani maana Itakuwa ni balaa jamani….. Ila kati ya watu wote bora hata Ivan ila Kinglawrence jamani asimsogelee mdogo wangu maana huyu kaka akili zake anazijua mwenyewe…hahahahhahahaha….Ila nampenda sana King but nisingependa kuona anamdate mwanamke yoyote nnaempenda au kumtakia mema maana akili zake na za Kenzo zimepishana kidogo tu….hahahahahahahaha….

Kama anachukulia na boss Ivan pia itakuwa sio poa kivileeee kutokana na situation yenyewe ila ni waaaaaaaay better than kuchukuliwa  Ommy Dimpoz au KingLawrence……

Mara KINGLAWRENCE akarusha hii video ya yeye na Ivan eti wanacheki  picha ya mtoto Wema kwenye

simu….Mweeeeehhhh… Nimechoka kabisaaa……

Mdau wewe umeisoma hii picha??? whats happening huko SAUZI jamani.????

PS: All in all, kama Ivan anamchukua Wema uwiiiiiii mbona wata break the internet sasa?? 

UPDATE:

BP ya umbea inapanda na kushukaaaa…….Mpaka nimesahau matatizo yangu kwa muda….hahhahaha

 Hii picha Kinglawrence aliirusha insta alafu akaifuta fastaaa kumbe mzee mzima Dougimasta16 alikuwa keshaicopy zamaniii….

Ndo kama hivyo mtoto sepenga katulia pembeni ya mzee Mzima Ivan president wa Richgang…..Alafu wote wamepiga black…

Jamani hii movie steling sijui nani???uwiiiiiiiii…… NIMECHOKAAAAAAAAAAAAAAAA…..

Uwiii sasa itakuwaje hapa jamani? Uwiiii So Wema ndo ataanza drive ile Lambo???? hahahha, uwiiii Zari asije zaa premature tu……

Akienda fata watoto ndo anamkuta yule yule aliekuwa anamtambia Africa nzima na bwanake ndo kasimama mlangoni na Khanga moja.??

Akituma message za kuomba big money ndo atajibiwa na mtoto sepetu???? Mie naona sio fresh Wema kuwa na huyu jmaaa ila kama jamaa ana mshiko mrefu kweli sioni tatizo aiseee, ila isiwe ana hela za kubadilisha mboga tu akampotezea muda… Yani afanye ya maana sasa amfungulie na Wema ma Jewelery store manini na nini yani mpaka Wema awe bosslady maana mtoto kanyanyaswa huyu jamani, kimtaji cha milioni 5 anasimangwa mpaka….. hahhahahahah

Uwiiii jamani watu wasije zaa premature…..hahhahahahahaha,,,,,,,,,

Read More

DEEP MAWAZUUU…..

Wapenzi naomba mniruhusu kuchukua sometime off blogging, ili niweze kudeal na 

some issues in my personal life……Maana nahisi mambo yanazidi kuwa mazito sasa…….

Inshallah, soon mambo yatakaa sawa na maisha yataendelea…..

Really, Im going through a lot right now. Niwekeni kwenye sala zenu niweze malizana na hii ngwee….

Yes, mambo yakishatulia ntakuja kuwaeleza kinaga ubaga chooote, kuanzia A-Z, tena in details….

Maana naamini you guys have earned the right to know the shitty side of my life too….Haitokuwa sawa kuwaonyesha the awesome side of my life only huku naficha the bad side……….Ila ngojeni mambo yatulie kidogo….. Yani wala sijali about haters anymore, wafurahi ,wanune, watajijua wenyewe. Nachokifanya ni kwa ajili yangu na watoto wangu mengine yote hayana uzito kivileeee…..

Keep me in your prayers……

Wateja wangu wa hollywoodshopaholics, naomba mnipe 1 more week ya kutuliza akili then I WILL BE BACK KAZINI…. Kila mtu atakuwa sorted out. Wenye kudai refund utapewa. Wa mizigo, mingine nimetuma jana. Wa corsets naomba muwe na subra nasubiria kiwandani wanitumie…. Please msiwe na wasiwasi na pesa zenu kila mtu atakuwa sorted out… Just one more week please…..By next week Wednesday ntaweza kuanza kudeal na biashara again…..

PS: Naomba nisichokozwe kwa muda huu, maana nna stress za ajabu, unaweza niita mjinga mwenzio nkakuchoma kisu, watu wakashaangaa yule kuitwa mjinga tu ndo kachoma mtu kisu kumbe nna mastress yangu mengine mengiiii….lol… So huu ni muda muaafaka wa kukaa mbali na mimi maana naweza kukumalizia hasira ambazo wala hazikuhusu….lol…

Read More

SHILOLE KUMCHAPA MAKOFI HUBBY-TO-BE…..NIMECHEKAAAA

Okay, there is nothing funny about domestic violence ila jamani ukisikiliza hii clip lazma uchekeeee mpaka ugale gale…

Jamani nimechekaaaaa, its soooo funny…. Naombeni msikilize mwishoni wa clip ambapo wanaume wanahojiwa kuhusu mwenzao kuchapwa makofi na mwanamke…hhahahahhahaha,, its soooo funny…. Eti mziwanda vumilia tu ila usitoke ndani ya hiyo nyumba pana maisha  hapo….hahahhahahahhahah….

KUSIKILIZA HIYO CLIP BONYEZA HAPA…..

Hii situation ndo ile ile ya Dida mchops na EZDEN, jamani mwanaume asie na hela anauziiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Unaweza kujikuta unakuwa kichaaa,kumbe ni hasira za kuwa na mtu asieku spoil…. Mkisikiliza clip kila mtu anamlaumu Shilole kwa kufanya fujo na kumpiga mtu wake mbele za watu….. Jamani heshma ya mwanaume ni pesaaaaa asikwambie mtuuu…… Huyu Nuhu atakuwa anachapwa vibao na mke wake kila siku…. Imagine hapo kamchapa mbele za watu wakiwa kwao si anamtandika daily…. Alafu sasa analeta wivu…..Shilole ndo anapata hasira zaidi ,pesa huna alafu hutaki niongee na wanaume wengine…hahaha…

si mnawajua wanaume wasio na pesa walivyo na wivu, uwiiiiii.. Atajifanya anakupenda kuliko alivyokuwaga anampenda mamake utotoni…. Huyo wivu sasa utajutraaaa…… Sasa mtu unamtegea mwanamke wako kula alafu bado unaleta wivu sasa unataka apate wapi hela…Mwache akatafute akuletee ule ila acha wivuuuuuuu…..hahahahahhaha….

Kama ushauri niliompaga EZDEN siku zile ngoja nimpe na huyu Nuhu. Kama unataka heshima ya mwanaume ndani ya nyumba chukua mwanamke mwenye kipato cha chini zaidi yako….. Nenda hata kijijini kwenu kachukue umlete town, huyo ukimpa hata elfu 10 atakupigia magoti na utapata ile heshma ya baba mwenye nyumba…Ila hapa kwa Shilole utaambulia kudhalilishwa tu kila siku……Jikaze we mtoto wa kiume bwana, usipende vya bure na hivyo vinaku costi…Ona una lia machozi mtoto wa kiume… Ungekuwa una hela zake hizo fujo alizoleta shilole ungemtwangaje makofi mpaka aone nyota? maana sio kwamba Shilole anakushinda nguvu za kupigana ila ni vile huwezi kumrudishia maana hujui utaenda lala wapi ukimpiga…Chapa lapa ,tafuta mwanamke utakaemudu wewe kama mwanaume. Hata kama unamuhonga elfu 5 tu, kuna wanawake wazuri sana hawana hata elfu 2 akikupata wewe wa kumpa elfu 5 atakuona ka Bhakhresa….Umarioo sio issue kabisa…

Shilole mdogo wangu… Clearly you will not be happy kuolewa na huyu jamaa….Yawezekana kuna part of you inampenda sana huyu jamaa ila the fact that hakulishi na hakuvishi itakuwa inakutia hasira kila siku…..Yani huyu hata akihema kwa nguvu utakuwa unapandwa na hasira…hahahhahahhaha…Sio lazma kuolewa mdogo wangu …Sometimes ni bora uwe single…. Ukishaona umefika sehemu unampiga vibao mchumba wako/mume wako mbele za watu ujue hakuna ndoa hapo…….Huna haja ya kuonyeshea watu kuwa unaolewa, olewa coz kweli umempenda jamaa…. Huku watu wanavunja uchumba harusi wiki ijayo… Huyu jamaa is not for you,,, Sio hata mambo ya age, mbona Mercy Galabawa yuko very happy na baba watoto wake na ni mdogo kwake more than 10 yrs. …Ni kwamba jamaa although ana age ndogo ila pesa yake imezeeka sanaaa….hahahhaha….. Asikwambie mtu mwanaume akiwa na hela ya maana hata awe na miaka 20 chini yako utamweshimu kama vile uko na mtu mzima wa miaka 50….hahahahha… Unaweza mwamkia mtoto mdogo….hhahahha…

Fact is the only time its okay and justified for a woman kulea mwanaume ni pale mwanamkw ushajizeekea,umechoka hakuna anaekutaka na wewe bado wataka malove dovey. Hapo ndo sawa ukachukue kimarioo chako ukiweke ndani ukilee….Ingawa kimarioo kinakuwa hakikupendi kivile ila poa tu, tena kikiangalia mwanamke tu unakichapa kibao….hahaa…. Ila kwa age na uzuri wa Shilole its doesnt make sense kulea mwanaume kwa kweli…Yeye ndo anatakiwa kulelewa na mwanaume….Huyu shilole 30 tu hajafika bado mtoto ni nini mambo ya kulea mwanaume….miaka 25 analea mwanaume Akifika miaka 60 huko je, usichezee ujana wako Shilole…..Bora uwe single lady ,upate tongozwa…ukishakuwa mke wa mtu ndo basi tena……hahahahhaha

Ukiwa na marioo utaonekana mwanamke kichaa,hana adabu anapiga mwanaume wake, kumbe wala sio hivyo … Alafu kinachoboa zaidi huwezi hata kusema tatizo ni nini ,inabidi tu useme hataki niongee na mtu ndo maana nimemchapa vibao….angekuwa ni mwanaume anaekuweka mjini ungemchapa vibao sababyu hataki uongee na mtu??? ….Jamani jikalieni single…Tena mkiwa single and available ndo rahisi zaidi kupata mwanaume unaemtaka wewe…..

Mkisikiliza hii clip kila mtu anamuona Shilole ni mwanamke kichaa na mwonevu….Msimuona Shilole ni mwanamke mshenzi au hana adabu….Shilole is a very good woman,,,Yani nampenda sana huyu mtoto toka nisome story ya maisha yake,jinsi alivyostruggle huko vijijini kupitia child abuse mpaka kufika hapo…In short Shilole ni mwanamke wa shoka…..IRONLADY HASWAAAA….. So msimuone chizi….Ni vile tu hawezi sema kinachomtia hasira……hahahhahaha…. Jamani  kuwa na mariooo ni shidaaaaaaaaaaa……….hahahahaha

Read More
1 2 3 132
Designed by muzemultimedia web design Tanzania